Kwa kawaida unaweza kutuma meseji katika mtandao wa WhatsApp kwa namba ambazo unazo katika kifaa chako mfano vile simu n.k
Mtandao wa WhatsApp bado unakua kwa ukubwa sana, na bado maboresha na vipengele vingi huwa vinaongezwa muda unavyozidi kwenda.
Pengine hauna haja ya kuwa na namba ya mtu, labda unataka uone kitu kidogo tuu alafu mmalizane labda unataka akutumie picha ya bidhaa kabla ya kufanya malipo n.k
Ndio, iko wazi kabisa kuna baadhi ya mazingira ambayo hayana ulazima wa kuwa na namba ya mtu katika simu yako—tena kama mazingira yenyewe ni ya mara moja moja sana
Njia Hizi Zitakuwezesha Kufanya Hivyo.
Tumia Kivinjari
Hapa unaweza ukaanzisha mazungumzo ya WhatsApp na mtu kwa kuingiza namba yake tuu katika kivinjari.
Unaweza fanikisha hilo kwa kuingia katika kivinjari chako na kisha andika wa.me/************ huku hizo sehemu zenye *** zikiwa zimeambatana na namba ya simu ya mtumiaji lakini hakikisha mwanzo unaanza na namba ya nchi mfano kwa Tanzania utaanza na 255
Baada ya hapo ukurasa mwingine utatokea ukurasa mwingine ukonyesha namba hiyo na kwa chini yake kutakua na maelezo yakisema ‘Continue to Chat’ gusa maneno hayo na kisha itakupeleka katika mtandao wa WhatsApp na kuanza mazungumzo.
Tumia Sehemu Ya “Message Yourself’
Ujanja mwingine wa haraka haraka ambao unaweza kuutumia ni kuingia katika eno la ‘message yourself’ na kisha jitumie namba ya mtu unaetaka kumtumia meseji ambaye hayupo katika simu yako.
Ukishajitumia utaona namba hiyo inaonekana kwa rangi ya bluu, hapo sasa unaweza ishikilia mpaka yatokee machaguo.
Katika machaguo hayo chagua neno “Chat With” likiwa limeambatana na namba hiyo ya simu ambayo unataka kuanzisha mazungumzo nayo.
Wewe unaijua njia gani? Niandikie hapo chini katika uwanja wa commnet, na vile vile nitonye, je nyia hizi ulikua unazijua? Ningependa kusikia kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.