Kama umezoea kutumia Microsoft Word na Excel kwenye kompyuta yako, utafurahi kujua kwamba teknolojia hii haijabaki nyuma na maendeleo ya intaneti. Sasa unaweza kupata huduma kama hiyo mtandaoni bure. Google Docs na MS Office Online ni kati ya programu kinara mtandaoni kwa kuandaa na kuhariri nyaraka (‘document’), ‘spreadsheets’ na hata ‘presentations’ mbalimbali kama unavyofanya na MS Office kwenye kompyuta yako. Programu hizi zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya hifadhi-pepe.
Ingawa uwezo wa Google Docs na Office Online hauwezi kufikia Programu za MS Office kamili kwa sasa ila, programu hizi zimetoka mbali na sasa zinaweza kufanya mengi kukamilisha kazi zako pale unapokuwa mbali na kompyuta ya ofisini. Programu hizi zinapatikana kwenye simu-janja, tableti na kwenye kiperuzi-wavuti cha kompyuta yoyote.
Programu hizi ni rahisi sana kutumia na itakuchukua muda mfupi kama umezoea kutumia MS Office. Kingine kizuri ni kwamba programu hizi zinafungamana na mfumo wa barua-pepe husika kukupa uwezo wa kuangalia nyaraka unazotumiwa na hata kuzihariri bila wasiwasi. Pengine faida kubwa ya kutumia huduma hizi ni uwezo wa kufanya kazi pamoja kwa wakati mmoja kati ya watu kadhaa pale mnapokuwa sehemu tofauti za dunia. Kila mmoja ataweza kuona yale mwenziye anaandika papo kwa hapo na kuweza kutoa maoni yake kwenye kurasa.
Ingawa Google Docs na MS Office Online zote zinafanya kazi ile ile, kuna utofauti kati ya huduma hizi mbili. Google Docs ni bure na bado inaendelea kukua huku ikisaidiwa na programu lukuki kutoka kwa watengenezaji washirika. MS Online pia nii huduma ya bure ila ina faida ya kufungamana na mfumo wa MS Office ambayo wengi wameizoea, kwa hiyo ni rahisi zaidi kujifunza. Ingawa MS Online ina uwezo wa kuridhisha, Microsoft wanatoa huduma yenye uwezo zaidi kama utaamua kulipia. Huduma hii inaitwa MS Office 365 na inakupa uwezo wa kutumia MS Office kamili popote – kwenye kompyuta moja, simu na tableti za Windows au I-pad. li kutumia Google Docs ama MS Online unatakiwa kuwa na akaunti ya Google au Microsoft.
Anza kutumia Google Docs au MS 360 sasa na tupe maoni yako kwenye facebook na twitter.
Kujifunza zaidi kuhusu google Docs, bofya hapa https://support.google.com/docs/#
Kujifunza zaidi kuhusu MS Office Online, bofya hapa https://office.com/start/default.aspx
No Comment! Be the first one.