Unaitumia vipi simu-janja yako, kupiga na kupokea simu tuu?. Inasemekana asilimia 80 ya watumiaji wa simu-janja hawatumii simu zao katika asilimia 100 kama inavyotakiwa. wengi huwa wanadownload vitu mbali mbali kama magemu na mitandao ya kijamii na kuingia katika intaneti tuu na wanakua wameridhika. vipi kama kuna vitu vingi unavyoweza tumia ukiwa na simu yako? Basi unakosa vitu vingi sana unavyoweza tumia ukiwa na simu-janja yako.
Sasa fahamu ya kwamba unaweza tumia simu yako kama vifaa vifuatavyo,
1. Tumia Simu-janja Yako Kama Redio Za Mawasiliano (Redio Kolu)
Aplikesheni kama zello (Android, iPhone/iPad,Windows) na HeyTell (iPhone, Android, Windows) zinasaidi kukuwezesha kutumia simu-janja yako kama redio kolu. zinakuwezesha kutuma meseji za sauti za kugusa na kuongea (push-to-talk) kama redio kolu za ukweli
2. Tumia Simu-Janja Yako Kama Kama Remoti Ya Kimataifa
Uamini au usiamini aplikesheni kama IR Remote (Android) na Dijit (iPhone) zinaweza kukuwezesha kutumia simu-janja yako kama remoti katika vifaa mbalimbali vya ki elektroniki. Kujua zaidi kuhusu kutumia simu yako kama remoti soma hapa
3. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wireless Mouse/Keyboard/Touchpad
Je ushawahi kuwaza kununua ‘wireless keyboard’ au ‘mouse’ lakini ukawa huna hela ya kutosha?. sasa mtandao kama Remotemouse.net unaweza ukakusaidia na ukashusha aplikesheni hiyo kwenye simu yako ya Android au iPhone na pia udownload Aplikesheni nyingine kwa kompyuta yako ili kutumia.
4. Tumia Simu-janja Yako Kama WebCam
Ushawahi kukaa na kufikiria kitu kama hiki (ha!). Unaweza usijue lakini ndio hivyo unaweza fanya simu yako ikawa WebCam ya kompyuta yako. Kuna Aplikesheni nyingi za bure kama WO webcam Lite (Android) na EpocCam (iphone) zinaweza kukusaidia kutumia simu kama webcam.
5. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wi-Fi Router
Hili linaweza lisikushangaze, simu nyingi za Android na iphone sasa zinakuja na Wi-Fi router ambazo zinaweza msaidia mtumiaji wa simu hiyo kurusha mtandao wa intaneti kwenye simu au kompyuta nyingine. ili kuwasha na kutumia mbinu hii nenda kwenye Wi-Fi Hotspot settings katika simu yako ya Android au iPhone
6. Tumia Simu-janja Yako Kama GPS
Simu nyingi siku hizi zinakuja na GPS kabisa, lakini aplikesheni kama GPS Status & Toolbox (Android) and Waze (iphone) zinaweza kukusaidia kutumia simu yako kama GPS kabisa.Aplikesheni hizo ni za bure katika Appstore na Google Playstore
7. Tumia Simu-janja Yako Kama Scanner
Mara ngapi umetaka ku scan nyaraka zako na ikakulazimu uende kwenye steshenali kwa sababu huna scanner? Kwa kutumia Aplikeshi ya simu yako kama CamScanner (Android, iPhone/iPad, Windows 8) huhitaji kuwa na mawazo kwamba utascan wap nyaraka zako. kitu kingine kuhusu aplikesheni hii ni kwamba ni ya bure na unaweza kuscan na nyaraka zako zikawa katika ubora wa hali ya juu
8. Tumia Simu-janja Yako Kama TV
KWa kutumia Aplikesheni kama LiveNow! TV (Android) and PBS (iPhone) unaweza kutumia simu yako kuangalia TV. Aplikesheni zote hizi ni bure katika masoko ya Android na Apple lakini unatumia Internet Kuangalia TV hiyo katika simu.
9. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wireless PC Speaker
Shusha Aplikesheni kama SoundWire (Android) or Airfoil Speakers Touch (iPhone, iPod, iPad) katika simu yako na kisha shusha software ya aplikeshi hizo katika komyuta yako. KWa kufanya hivyo hapo utaweza kucheza miziki katika simu yako kwa kutumia kompyuta
10. Tumia Simu-Janja Yako Kama Motion detector
Kama simu yako ina sensa, basi unaweza ukafanya mambo mengi ya kuvutia kama kubadili wombo katika simu yako kwa kupitisha mkono juu ya skrini bila kugusa simu. kama una uhakika simu yako ina sensa basi shusha Proximity Actions (Android) au Smart Player Free (iPhone) kutumia simu yako bili kugusa skrini.
Sasa nina imani unaweza kutumia Simu-janja zako kiujanja zaidi. Kama una wazo lolote ningependa kulisikia kuhusiana na hii makala, tuwasiliano kupitia akaunti zetu za Twitter au Facebook
No Comment! Be the first one.