Kulikuwa na njia mbalimbali zisizo rasmi za kutumia WhatsApp kwenye kompyuta lakini sasa WhatsApp wamekuja na njia rasmi!
Kama wewe ni mmoja wa watumiaji milioni 600 wa WhatsApp hii ni habari nzuri kwelikweli kama huwa unajikuta kazini unapata shida kila saa kutazama simu yako ili kujua umetumiwa nini. Hii ni habari njema kweli kweli kwa wafanyakazi na wengine wengi wanaokuwa wanatumia kompyuta kwa muda mwingi wa siku.
Je unaitumiaje?
Kwanza hakikisha unatumia toleo jipya kabisa la WhatsApp, nenda kwenye soko la apps kwenye simu yako kuhakikisha hilo.
Hatua
1. Kwenye kompyuta yako, fungua Google Chrome kisha nenda https://web.whatsapp.com
2. Utaona kodi ya QR
Android/Windows/Nokia S60
3. Fungua app ya WhatsApp, Nenda Menu, Chagua WhatsApp web.
Simu za BlackBerry
3. Fungua app ya WhatsApp, Nenda Chats, Bofya Menu, Chagua WhatsApp web.
4. Kisha onesha simu yako kama vile unapotaka kupiga picha eneo la kodi ya QR kwenye https://web.whatsapp.com
Kutokana na vikwazo vilivyo kwenye simu za Apple (iPhones) bado wenye simu hizo hawataweza kutumia huduma hii kwa sasa. Pia kwa sasa hutaweza kutumia huduma hii kwenye Firefox, Internet Explorer na zingine zaidi ya Google Chrome tuu.
Endelea kusoma Teknokona, usisahau kusambaza makala hii kwa ndugu na marafiki!
One Comment