Tumeshaandika sana kuhusiana na simu za kujikunja na kukunjua, ni wazi kwa sasa soko la simu janja hizo (Fold) linakua kwa kasi sana, na makampuni mengi wanataka kuwa sehemu ya soko hilo Google Pixel nao hawataki kubaki nyuma.
Soko la Simu za kujikunjaa kwa sasa maarufu kama Fold limeshikiliwa na kampuni ya Samsung ambayo kwa mara ya kwanza ilikuja na simu ya aina hii mwaka 2019 lakini je uko tayari kwa toleo la Google Pixel Fold?
Baada ya Samsung kuingia katika soko hili watengenezaji wengi wa simu za Android na wenyewe walingia katika soko hili, makampuni kama Motorola na mengine yaliingia katika soko hili.
Kampuni ya Apple yenyewe mpaka sasa haijaingia katika soko hili hata Google nao bado hawajaweka bidhaa ya namna hii katika soko lakini kuna mengi yanaongelewa chini chini –kwa muda mrefu—kwamba makampuni haya yanaleta kifaa hivi karibuni.
Turudi kwa Google Na Simu Janja Ambayo Inategemewa Yaani Google Pixel Fold.
Inasemekana kwamba Google wameanza –kimya kimya—kuandaa simu janja ya aina hii tanfia mwaka 2018 lakini ubaya ni kwamba haijawahi kufanikiwa kuingia sokoni huku sababu zikiwa ni nyingi tuu.
Kama unakumbuka vizuri mwaka 2019 walisema wanashughulikia kuwa na simu janja ya aina hii, simu ambayo waliipa jina lisilo rasmi la ‘Passport’.
Muda ulipita na mpaka sifa za undani za simu hii zikaanza kuonekana katika baadhi ya vyanzo kama sehemu ya fununu lakini cha kushangaza haijawahi ingia sokoni.
Kitu ambacho kilifanyika ni kwamba kampuni iliachana na kifaa hicho –passport—na kuhamia na kuanza kuandaa kifaa kingine ambacho walikipa jina la ‘Pipit’ ambalo sio rasmi.
Hapa watu wengi walitegemea kuwa watapata toleo la Google Pixel Fold lakini mambo hayakua kama kusudio lao.
Hapa tena kampuni ikaachana kabisa na ‘Pipit’ na ikaenda mpaka kuwa na kifaa kingine ambacho wakakipa jina la ‘Felix’
Na mpaka kufikia hapa inasemekana kuwa kampuni imeshapata toleo ambalo imaridhika nalo kabisa na wanahisi litaweza kuleta ushindani katika soko.
Kwa sasa simu janja za Pixel zinafanya vizuri sana katika soko huku sifa (specification) zake za undani zikiwa ni za hali ya juu sana, vivyo hivyo inavyotegemewa kwa Google Pixel Fold.
Mpaka sasa hakuna muda rasmi ambao kampuni itautumia katika kuzindua simu janja hizo na kuingizwa sokoni—hatuna budi kusubiri.
Kaa tayari kuangalia kitu katika kioo –Google Pixel Fold– kidogo na kukihamishia na kuendelea nacho katika kioo kikubwa kwenye kifaa kimoja kutoka Google.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.