Ni wazi kwamba Samsung ni moja kati ya makampuni ambayo ina matoleo mengi sana na kwa mwaka huwa wanatoa simu janja nyingi sana pengine ukilinganiasha na kampuni zingine nyingi kubwa katika soko la simu janja.
Na kwa sasa ni kwamba kuna kampuni nyingi ambazo ziko katika mchakato wa kuachia simu zao –tena zile zenye ushindani wa hali ya juu—katika soko na Samsung hawako nyuma.

Makampuni kama OnePlus, Motorola nao wametangaza kuachia simu zao hivi karibuni na Samsung Galaxy S23 Ultra nayo iko mbioni.
Kama toleo lake la nyuma, Galaxy S23 zitatoka katika matoleo matatu mwezi februari, matoleo hayo ni Galaxy S23, Galaxy S23 Plus na Galaxy S23 Ultra.

Lakini katika mtandao wengi wanaongelea sana toleo la Galaxy S23 Ultra, na ndilo ambalo naenda kuligusia kidogo ili tujue tarehe ya uzinduzi na sifa za undani.
Galaxy S23 Ultra in Cream. 👀
I think it looks great in person. pic.twitter.com/k1rLT7EXAr
— Alvin (@sondesix) January 22, 2023
Inayosemekana kuwa ni tarehe ya uzinduzi wa simu hizo ni tarehe 1 mwezi wa pili mwaka huu na mpaka sasa bado Samsung hawajaachia sifa za undani kuhusiana na simu hizo lakini tunahisi ni kama zifuatazo.
S23 Ultra itakua na chip ya Qualcomm Snapdragon 8 Gen 2 chip, RAM yake inaweza ikawa GB 8 au 12 Betri kubwa tuu la uwezo wa 5000mAh.

Kioo chake kinaweza kikwa na ukubwa wa inchi 6.8 na chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED 2X na uwezo wake wa Pixel ni 501 PPI.
Kwenye kamera sasa! Ni kwamba inakuja na kamera nne – kamera kuu itakua na 200MP, 12MP ikiwa ni kwa ile kamera ya kuchukua eneo kubwa (Ultrawide), 10MP ikiwa ni ile ya telephoto ikiwa na uwezo wa kuvuta hadi 10X na vilevile kamera nyingine ambayo ina 10MP na ina uwezo wa kuvuta hadi 3X huku na yenyewe ikiwa ni ya telephoto.
Teknolojia ya telephoto katika picha ni teknolojia ambayo inasaidi katika kuchukua picha kwa vitu ambavyo viko katika umbali mkubwa.

Ukichana na sifa hizo hapo kuna sifa za kawaida sana siku hizi katika simu janja tena zile shindani katika soko, vitu kama Fast charge, kuchaji bila waya (Wireless Charging), kuzuia kwa maji kuingia n.k vitakuwepo katika baadhi ya sifa za simu hii
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi kuna sifa unadhani itakuwepo kwenye simu hizi na nimeiacha?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.