Mchezaji aliyekuwa na mkataba kuchezea timu B ya mpira ya Barcelona FC ya nchini Uispania ajikuta hana ajira siku chache baada ya kupata mkataba huo na uongozi wa timu ya Barcelona kugundua tweet yake ya zamani.
Wengi wanasema ubaya mmoja wapo wa ulimwengu wa mitandao ya jamii tuliopo sasa ni ugumu wa kukumbuka na kufuta vitu tulivyokwisha kuviandika katika mitandao hiyo, na hili linaonekana litakuwa limemuumiza sana kijana Sergi Guardiola.
Kijana Sergi mwenye umri wa miaka 24 alifanikiwa kusaini mkataba na kutambulishwa rasmi jumatatu asubuhi, kufikia jioni mkataba wake ukawa umevunjwa.
Je tweet yake ilisemaje?
- Alisifia Real Madrid na kumtusi shabiki wa FC Barcelona
Inaonekana kipindi cha miaka ya nyuma kijana huyu alikuwa mpenzi zaidi wa timu ya Real Madrid na kupitia twitter alimtusi shabiki ya timu ya FC Barcelona kwa kumuita malaya wa Catalonia, nyumbani kwa timu ya FC Barcelona.
Na masaa machache baada ya Serge kupata mkataba katika timu hiyo tweet yake ya mwaka juzi (2013) ilifika kwenye macho ya mabosi wake wapya na kufikia jioni mkataba wake ukawa umevunjwa.
Serge amejitetea kwa kusema ya kwamba tweet hiyo haikutumwa na yeye bali na rafiki yake lakini bado ni jambo lisiloiingia akilini na inaonekana ni njia ya kujitetea tuu baada ya kukosa kibarua.
TeknoKona inakushauri kupitia akaunti yako kijamii mara moja baada ya kufanya uamuzi wa kuomba kazi katika kampuni au shirika ambalo unauhakika ushawahi kuongea dhidi yake. Na pia kumbuka matusi sio dili mtandaoni, kuna siku yanaweza kukuathiri.
Je una maoni gani juu ya hili? Kumbuka kuungana nasi kwenye mitandao ya kijamii na pia kusambaza makala kwa marafiki.
No Comment! Be the first one.