Kama ulikua unategemea Twitter iongeze idadi ya maneno katika Tweets, ondoa wazo hilo kwani hilo halitawezekana tena
Hapo awali Twitter walitoa ripoti kuwa wanafikiria kuongeza idadi ya maneno katika Tweets watu watakazokuwa wanatuma. Namba ambayo ilifikiwa ni kwamba kampuni ilikua inafikiria kuifanya tweet moja iwe hadi na herufi 10,000 (ni herufi nyingi sana kwa Twitter niliyoizoea)
Mkurugenzi wa mtandao huo wa kijamii Bw. Jack Dorsey ametoa taarifa hizi ijumaa iliyopita (18/03/2016) kuwa Mtandao huo hauna mpango tena wa kuongeza idadi ya maneno katika Tweets zitakazo kuwa zinatumwa.
Kumbuka umaarufu wa idadi chache ya maneno katika Twitter (herufi 140) ndio umechangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa kwa vifupi vingi vya maneno kama vile OOMF,FF na vingine vingine. Maneno yakiwa mengi kwa mtazamo wangu Twitter inaweza ikapoteza utamu wake (kama unanielewa)
Kwa wengine hii inaweza ikawa si habari njema kwako kwa wanapata shida kutuma Twitter nyingi wakielezea kitu kimoja. Wengine katika kujielezea kwa ufupi hawawezi na idadi kubwa ya herufi zingewasaidia. Mpaka leo kuna watu wanaandika Tweets zaidi ya moja katika kuelezea kitu kimoja tuu.
Hata hivyo kuna ujanja ujanja mwingine wa kutumia katika kuhakikisha unavuka herufi 140 katika Tweet. Kwa mfano unaweza ukapandisha picha katika Twitter na ukabofya sehemu ya “Who’s in this photo” ili kuwa ‘tag’ wale ambao wapo katika picha hiyo. Sasa badala ya kufanya hivyo unaweza ukaamua kuongeza maneno mengi tuu ambayo ulitaka kuandika ila herufi zikawa hazitoshi.
Japokuwa hii ilitupambaza wengi kwa kujua kuwa mabadiliko yatakuja. Lakini Bw. Dorsey amesema tusahau kabisa katika mabadiliko hayo na pia amesema Twitter moja kati ya malengo yake ni kuwasaidia watumiaji wake kutuma Tweet ili kuweka mawasiliano ya haraka haraka.