Upo uwezekano mkubwa Twitter inataka kuleta mabadiliko makubwa katika muonekano wake katika app yake ya Android, muundo mpya unalenga saana kuwavutia watumiaji wengi zaidi kwa kufanya utumiaji wa app hii kuwa rahisi zaidi.
Ni ukweli usiofichika kwamba watuwengi ukiwaauliza kwanini hawapo katika mtandao huu watasema kwamba ni kwasababu wanashindwa kuuelewa hii inawafanya wajiunge na kisha baada ya muda waache kuitumia, ugumu wa kutumia ndio umekuwa sababu kubwa kwa app hii kupata muundo mpya.
Inasemekana Twitter inakuja katika muonekano unaofuata sheria za ubunifu za Google – Material Design
Muundo huu mpya unaleta muonekano tofauti na ule tuliouzoea sasa watumiaji wataweza kuzipata kurasa za Timeline Moments Notisification Message na Profile kwa urahisi zaidi, ukiwa katika Timeline ambapo ndipo mtumiaji anapoweza kuona tweets ama vibandiko kutoka kwa watu anaowafuata basi kwa ku-swap kwenda kulia utakuwa katika ukurasa wa mambo ambayo yanaongelewa zaidi wa Moments ukienda kulia tena basi utakuwa katika ukurasa wa Notification na ukienda kulia unaukuta ukurasa ambao unakuwa na Ujumbe.
Zaidi ya hayo sasa ukurasa wa akaunti ya mtumiaji sasa umewekwa karibu zaidi na kwa kugusa mara moja tu mtumiaji atapelekwa katika ukurasa wake kitu ambacho kingechukua muda kidogo kufikiwa katika mfumo tulio nao sasa hivi.
Mwisho katika muundo mpya hakuta kuwa na sehemu ya kuandikia vibandiko katika sehemu ya chini ya ukurasa kama ilivyokuwa zamani bali sasa kutakuwa na kitufe kimoja upande wa kulia ambacho utakapo kifungua basi kitakupeleka sehemu ya kuandika Tweet mpya.
Mabadiliko haya yameanza kuonekana kwa watu wanaotumia matoleo maalumu ya Twitter ya Android, upo uwezekano mkubwa kwamba mabadiliko haya yatakuja katika app za Android ingawa pia kuna uwezekano yasiweze kupitishwa kutumiwa katika app.
Teknokona inaimani mabadiliko haya yatawashawaishi watumiaji wapya “newbie” wengi kujiunga ama kurudi kutumia mtandao huu baada ya kuwa umerahisishwa muonekano wake.
Tuambie katika maoni yako unaonaje haya mabadiliko je yanakushawishi kujiunga na mtandao huo.
Vyanzo: The verge na mitandao mingine