Unakumbuka hapo nyuma tuliandika kwamba kwenye mtandao wa kijamii maarufu wa twitter, mtu yeyote anaweza kuomba kupata tiki ya bluu.
Tiki hiyo angeweza kuipata kwa kujaza fomu maalumu, na kisha akafanyiwa uhakiki na mtandao huu na baada ya hapo anaweza kuipata au asiipate kulingana na jinsi twitter wenyewe walivyoona.
Vile vile niliandikaga kuhusu twitter kutoa tiki ya bluu kimakosa na hii unaweza kuisoma zaidi —> Hapa <—
Sasa baada ya hili sakata mtandao huo umeamua kusitisha kwa muda zoezi hili la kutoa tiki ya bluu kwa muda.
We’ve temporarily hit pause on rolling out access to apply for Verification so we can make improvements to the application and review process.
For those who have been waiting, we know this may be disappointing. We want to get things right, and appreciate your patience.
— Twitter Verified (@verified) August 13, 2021
Sababu ya msingi ambayo mtandao huu unaitoa ni kwamba inasema imefanya hivyo makusudi ili kuhakikisha kwamba inakiboresha kipengele hiki.
Tuwape muda tuone itakuaje….
Naomba niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umeipokeaje?
Kumbuka Kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
No Comment! Be the first one.