‘VineKids’ ndio jina la App hii mpya ya twitter, ni sawa na vine tuu. Lakini hii inajikita sana kwa watoto kati ya umri wa miaka mitano hadi kumi na mbili. Baada ya App ya vine kuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wengi watoto ndipo twitter ilipoachia vinekids ijumaa ya januari 30. App hiyo mpya inajitegemea na inajikita zaidi kwa watoto na itakua inahusisha mambo ya watoto kama vile picha za katuni za kawaida na zile zinazoongea na picha za kuchekesha.
“Wazo lilikuja mwanzoni Januari, baada ya mazungumzo marefu ofisini amabapo mfanyakazi mwenzangu alikua akiongelea jinsi mtoto wake wa miaka miwili anavyoipenda vine” Alisema Carolyn Penner, mkuu wa mawasiliano na masoko wa vine
Kuona Vine nyingine mtoto atagusa simu yake ya tachi kulia kwenda kushoto (ikiwa ni ishara ya kusogea mbele). App inatoa sauti ya kufurahisha na haraka kila mara mtoto anapogusa kioo cha simu-janja yake.
Hizi video fupi za vine kwa ajili ya watoto zinakua zimechagulia na wahariri wa vine na watoto hawawezi ku rekodi video na kuisambaza katika vine. Pia hata hivyo watoto hawataweza kutengeneza Akaunti ili kuangalia video za sekunde sita katika vine. Video ambayo itakua imetumwa katika vine ya wakubwa haitatumwa kwa watoto. Hii inaepusha watoto kuona video ambazo hawapaswi kuona.
Twitter imefuata vigezo na masharti yote ya kimtandao yanayohusu watoto kupitia Children’s Online Privacy Protection Act (COPPA) katika swala zima la kutengeneza vinekids.
Vinekids imesema hata hivyo haitachukua taarifa za siri za watoto labda zile ambazo wazazi wamejitolea kutoa wenyewe kwa vine. taarifa zinazochukuliwa ni jina, barua pepe na taarifa zingine ambazo mtu atakubali vinekids kuwa nazo.
Haiko wazi ni nini twitter imepanga kufanya na Vinekids lakini kilicho wazi ni kwamba mtandao mpya unafanya juu chini kutafuta njia mbali mbali za kutoka na kuwa juu zaidi (Unaweza Sema Kama TeknokonaDotCom Vile) kwa kuongeza watumiaji na kuongeza mapato. Ikifanikisha hili hatimaye hata wawekezaji watakua na furaha kwa kua matunda yanaonekana.
Kama Vine Kids itapata mafanikio makubwa, basi itaongeza watu wengi ambao watajiandikisha katika vine ya toleo la wakubwa na itaongeza ufikio mkubwa wa twitter duniani.
Msomaji wetu tafadhali Tembelea na kurasa zetu zingine za Twitter, Facebook Na Instagram
No Comment! Be the first one.