Mtandao wa Twitter umeanza majaribio ya stika katika picha ikiwa ni muendelezo wao wa kupambana kuongeza watumiaji wapya, baadhi ya watumiaji wa Twitter wameripoti kuona kitu hicho kipengele hicho kinacho kuruhusu kuongeza stika katika picha kabla ya kuposti.
Kama ulikua hujui kwa kipindi cha karibuni Twitter imekuwa iko katika wakati mgumu baada ya thamani yake katika soko la hisa kushuka, hii inasababishwa na mtandao kushindwa kuendelea kukua kwa kupata watumiaji wapya wengi. Hatua nyingi zimechukuliwa na bodi ya wakurugenzi kuinusuru Twitter na baadhi ya mambo waliyofanya ni kumrudisha Mtendaji mkurugenzi ambaye pia ni mwanzilishi Jack Dorsey ambaye alipokuja alifanya mabadiliko makubwa kama vile ilie la mtindo wa timeline.

Kuleta stika katika Twitter kutakuwa na maana moja tu nayo ni kwamba Twitter wanapenda kutuona tunashare picha nnyingi zaidi katika mtandao kitu ambacho kitatufanya tuwe re-tweeted zaidi na kupata likes nyingi zaidi ila yote haya yatapelekea mtandao kukua zaidi.

Kwa maana kwamba kama majaribio haya yatapita maana yake ni kwamba watumiaji wa Twitter watakuwa na uwezo wa ku share picha ambazo zina stika mbali mbali kama vile kopa, hii itaifanya Twitter izidi kufanana na mitandao mingine inayofanya vyema.
Pamoja na kuwapa uwezo huu watumiaji katika picha pia watakuwa na uwezo wa kuangalia jinsi watumiaji wengine ambavyo wameirekebisha picha hiyo hiyo, pia pindi unapo tumia stika moja utakuwa na uwezo wa kuangalia picha nyingine ambazo pia ungeweza kutumia stika kama hiyo.
Ingawa Twitter imekuwa inafanya jitihada za makusudi ili kuokoa thamani ya share zake, lakini bado thamani ya hisa za Twitter zimekuwa zikishuka tunategemea labda juhudi hizi zinazofanyika sasa zitakuwa na matokeo baada ya muda mrefu.
Chanzo: Mtandao wa RECODE na mitandao mingine