Picha na linki hazitahesabiwa tena katika jumla ya herufi 140 ambazo ni kikomo cha idadi ya herufi katika tweet moja.
Zamani utumiaji wa linki za tovuti pamoja na picha au video zilikuwa zinahusisha pia na upunguaji wa idadi ya herufi unazoweza andika kufikia kikomo cha herufi 140.
Mkurugenzi wa Twitter Bwana Jack, tayari alisema yupo tayari kufanya maboresho kadhaa madogo madogo na makubwa katika mtandao huo wa kijamii maarufu ili kuhakikisha unaendelea kuwafanya watumiaji wake kuendelea kuufurahia. – na pia kuvutia watumiaji wapya.
Mabadiliko haya ni muhimu na ni moja ya maboresho yaliyokuwa yanaitajika kwa wengi ila bado hawajaleta badiliko moja kuu ambalo linadaiwa sana na watumiaji wake. – Kufanya maboresho ya tweet uliyokwisha ituma kwenye mtandao huo…yaani ‘kuedit’! Hadi sasa kama umefanya makosa kwenye tweet uliyokwishaituma basi hauna budi kuifuta kabisa kabisa na kuituma upya.
Je wewe ni mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter? Je unayoona vipi mabadiliko/maboresho haya?
Vyanzo: TheAntlantic.com na mitandao mbalimbali