Twitter ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo ina nguvu sana katika jamii, licha ya mtandao huo kuwa hivyo bado unazidi kujiboresha kwa kuongeza vipengele kadha wa kadha na kwa sasa ni eneo la video.
Japokua mitandao mingi ya kijamii kwa muda tuu imekua ikitumia kipengele hichi kwa muda tuu, kipengele chenyewe kinahusisha video kuonekana kwa ukubwa ambao unafunika karibia uso wote wa kioo cha simu, Twitter nao wameona wasibaki nyuma.
Kinachofanyika hapa ni kwamba, mtandao utakua unaonyesha video fupi fupi zikiwa katika mpangilio kama wa video za TikTok, zile za Reels ndani ya Instagram au hata zile za Shorts za Youtube.
Kipengele hichi ni kwa watumiaji wote yaaani wale wa Android na iOS. Kwa sasa mitandao mingi ya kijamii inajikita sana katika kuhakikisha kuwa ina mfumo mzuri katika eneo la video.
Ili kufikia katika jukwaa hili na kuweza kuona video mbalimbali kwanza itakubidi uguse video moja wapo ambayo unaitaka kuiangalia katika Tweet, na kisha utafunguku ukurasa wenye video yako na kwa chini kutakua na video zingine ambazo unaweza endelea kuziona.
Kama utaangalia video nyingi na ukaridhika ukirudi nyuma tuu basi utarudi katika Timeline yako ya twitter na kuendelea na mambo mengine.
Kwa sasa kipengele hiki kipo katika hatua za maandalizi na majaribio, bado haiko wazi juu ya lini kitaanza kupatikana kwa wote, lakini nadhani hakitachukua muda.
ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie katika eneo la comment je hii umeipokeaje? Je unadhani ni sawa kwa Twitter kuja na kipengele hichi kwa sasa wakati wengi wakisema wanaiga?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.