Pengine unaweza ukawa unajiuliza ‘Closed Caption’ ni nini? Kwa uharaka haraka ni ule uwezo wa kutazama video huku unapata maandishi kwa chini? Kitu ambacho hapo awali Android na iPhone hazikuwa nacho katika App ya Twitter.
Ikumbukwe kuwa huduma hii sio mpya maana mwaka jana mwishoni ndio ilizanza kupatikana ila katika Twitter ya mtandao tuu
Huduma hii sio ngeni kwa baadhi ya mitandao ya kijamii kama vile Youtube, maana wao wana huduma hii kwa kipindi cha muda mrefu sasa.
Vile vile huduma hii huwa na uwezo wa kufanya tafsiri kupitia lugha mbali mbali yaaani unaweza ukawa unatazama video ambayo wanaongea kzungu lakini ukawa unapata maandhi ya kichina kwa pale chini
… inategemea na wewe ungependa kusoma maandishi kwa lugha ipi? Hili ni jambo zuri sana kwa mtandoa wa kijamii wa Twitter inaonyesha ni jinsi gani inawathamini watumiaji wake.
Sasa basi katika video kwenye Android au iOS kupitia Twitter kipengele hiki kitakua kikionekana upande wa kulia kwa juu kabisa ya video hiyo na kitakua na alama ya ‘CC’
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, hii umeipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.