Mtandao wa Twitter umeanza kutumia algorithm katika timeline kimya kimya kuanzia tarehe 15 yaani juzi, makala hii pamoja na yote itakufundisha jinsi ya kuzima algorithmic timeline na kuendelea kutumia reverse chronological order timeline.
Je algorithmic timeline ni nini hasa!?
Tunaposema kwamba Twitter wameanza kutumia algorithm ama algorithmic timeline tunamaana kwamba Twitter sasa wameanza kuamua ni tweets zipi wewe uzione pindi unapofungua ukurasa wako wa Twitter, zamani walikua wanatumia utaratibu wa reverse chronological order timeline ambao ulikua unazipanga tweets kutokana na muda ambao watu unaowa follow walitweet hivyo zamani tulikua tunaweza kuona tweets kutoka mtu yeyote awe ni bigwig ama side z ??.
Ingawa wakati Twitter wanatambulisha huduma hii walisema kwamba huduma hii mpya ya algorithmic timeline itakuwa kwa wale tu ambao watataka lakini leo Teknokona imegundua kwamba watumiaji wote wa Twitter wamepewa algorithmic timeline ila tu kwa wale ambao hawaitaki wanaweza kubadili mpangilio na kuendelea kutumia utaratibu wa zamani.
Jinsi ya kubadili mfumo ili kutumia mfumo wa zamani
Kama unatumia simu ya Android
- Unaenda katika sehemu ya overflow ni sehemu iliyo juu kulia ukiwa katika Timeline yako
- Kisha unaenda sehemu ya Settings.
- Ukiwa Settings nenda sehemu ya Timeline.
- Ukiwa katika Timeline utaona maneno “Show me the best tweets first” ondoa pata katika kibox kilichopo mbele ya maneno haya. Hapo utakuwa umerudi kutumia njia ya zamani ya timeline.
Kama unatumia simu ya iPhone ama iPad.
- ukiwa katika profile yako nenda katika kitufe cha gea ambacho huwa kinakuwa chini ya picha ya cover
- Ukiwa hapo chagua Settings
- Chagua akaunti ambayo unataka kuifanyia haya marekebisho
- Chagua Timeline Kisha chagua Timeline personalization.
- Ukiwa hapo utaona maneno “Show me the best tweets first” ondoa pata katika kibox kilichopo mbele ya maneno haya. Hapo utakuwa umerudi kutumia njia ya zamani ya timeline.
Kama unatumia twitter katika kompyuta au mtandao
- Fungua Twitter kwa kubofya hapa
- Ingia katika akaunti yako.
- Fungua sehemu ya Account settings
- Tafuta Content
- Ndani ya Content tafuta maneno “Show me the best tweets first” ondoa pata katika kibox kilichopo kabla ya maneno haya. Hapo utakuwa umerudi kutumia njia ya zamani ya timeline.
Ni matumaini yetu kwamba umeelewa maana hasa ya algorithmic timeline na pia reversed chronological order timeline na tunatumaini kwamba utachagua unachopenda na kuendelea kufurahia Twitter.
Vyanzo: The next web pamoja na vyanzo vingine mtandaoni.