Twitter ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo ina nguvu kubwa sana ukilinganisha na mitandao mingi tuu, hata watumiaji wake wengi hutofautiana tabia za kimtandao na watumiaji wa mitandao mingine.
Kwa sasa Twitter imefanya upendeleo kwa watumiaji wa iOS na wamewaletea kipengele kingine kipya cha Picture-In-Picture.
Kipengele hiki sio kigeni duniani maana kuna mitandao mingi inaruhusu kipengele hiki. Kwa haraka haraka ni kwamba kipengele hiki kinahusu kunagalia video kutoka katika mtandao, huku ukiwa unafanya mambo mengine kama vile kujibu meseji n.k
Hii inamaanisha wakati unaangalia video kupitia mtandao huo sio lazima ubaki humo humo katika App hiyo ili kumalizia hiyo video….. unaweza ukatoka na bado ukawa unaangalia video hiyo huku unafanya mambo mengine.
Looks like Twitter videos now support the iOS system wide PiP.
Note that it’s rolling out slowly, so it’s normal if some of you don’t have it yet pic.twitter.com/QeCrI670XA— iSoftware Updates (@iSWUpdates) June 30, 2023
Mpaka sasa wengi walikau na uwezo wa Picture-In-Picture wakati wako ndani ya App (ya Twitter) tuu kwamba utaweza zunguka ndani ya App humo humo wakati unaangalia video hiyo.
Lakini kwa sasa utaweza hata kutoka ndani ya App hiyo na kufanya mambo mengine mengi tuu wakatika ukiangalia video hiyo kutoka katika mtandao wa Twitter.
Kingine ni kwamba kipengele hiki kitaanza kuachiwa taratibu mpaka kumfikia kila mtu ambae anatumia kifaa cha iOS.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya comment, je unadhani ni sawa kwa mtandao kuongeza vipengele vingi hivi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.