Twitter wamteua mdukuzi maarufu kuchukua cheo cha usalama wa data katika usimamizi wa huduma ya mtandao wao wa kijamii. Bwana Peiter Zatko anatambulika kwa jina la Mudge katika ulimwengu wa usalama wa data na udukuzi.
Bwana Peiter katika nafasi hiyo ya Mkuu wa Usalama wa Kidigitali amepewa mamlaka mapana ya kupendekeza mabadiliko ya aina yeyote katika kampuni hiyo yatakayoboresha usalama kwenye huduma ya Twitter. Peiter atakuwa anafanya kazi chini ya muanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Jack Dorsey.

Uamuzi huu unaonekana kuchochewa na matukio kadhaa ya udukuzi yaliyotokea hivi karibuni. Akaunti za watu muhimu na maarufu zilidukuliwa na kutweet vitu visivyokuwa vya usalama, udukuzi huo ulihusisha akaunti kama vile ya Elon Musk, Bill Gates, Uber, Apple, Barack Obama na msanii Kanye West.
Zatko hivi karibuni alisimamia usalama katika malipo ya elektroniki. Kabla ya hapo, alifanya kazi kwenye miradi maalum katika Google na alisimamia kutoa misaada kwa miradi ya usalama wa kimtandao katika Kituo cha Utafiti wa Juu na Utekelezaji wa Mradi maarufu wa Pentagon (DARPA).
Zatko alianza kazi miaka ya 1990, wakati huo huo alifanya kazi ya siri kwa kontrakta wa serikali na alikuwa miongoni mwa viongozi wa Cult of the Dead Cow, kikundi cha udukuzi mashuhuri kwa kutoa zana za utapeli za Windows ili kumshawishi Microsoft katika kuboresha usalama.
No Comment! Be the first one.