Katika mtandao wa kijamii wa Twitter eneo la Direct Message huwa linaonekana katika ukurasa wa mtumiaji wa mtandao huo.
Eneo hilo katika mtandao wa Twitter ni mahususi kwa ajili ya kutuma ujembe kwa mtu moja kwa moja kupitia katika ukurasa wake (profile).
Ni wazi kuwa mtandao wa kijamii wa Twitter umekua na mabadiliko ya hapa na pale mara tuu baada ya mtandao huo kununuliwa na bwana Elon Musk.
Mpaka sasa yameshafanyika mabadiliko mengi sana na ni wazi kuwa kuna mengine mengi yatakuja kadri muda unavyozidi kwenda.
Kumbuka madadiliko ambayo yanafanyika huwa yanaathiri pande zote mbili yaani katika upande wa wafanyakazi na hata watumiaji wa mtandao huo wa kijamii.
Tulishaandika >>HAPA<< juu ya kampuni hii ilivyopunguza baadhi ya wafanya kazi na hii ni baada tuu ya bwana Elon Musk Kuwa bosi wa mtandao huo wa kijamii.

Kuna taarifa nyingi za malalamiko zimekua zikienea katika mitandao, watumiaji wa Android wakiwa wanalalamika kuwa katika App ya Twitter eneo hilo limetoweka.
Hata kwa baadhi ya watumiaji wa iPhone wamekua na lawama za aina hiyo hiyo lakini cha kushangaza ni kwamba jambo hili halijatokea kwa watumiaji wote wa iOS.
Kumbuka zamani eneo la Direct Message (DM) lilikua linatokea pembeni ya neno Following au Follow katika ukurasa wa mtumiaji wa mtandao huo.
Kazi yake ilikua ni kurahisisha tuu mawasiliano yale ya njia ya ujumbe mfupi wa siri, kwa wale watumiaji wa twitter ya kivinjari bado wanaweza kupata huduma hii kama kawaida.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je kwa upande wako tatizo hili umekutana nalo? Je unadhani kuna madabiliko gani mengine yanaweza kutokea katika mtandao huo wa kijamii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.