Twitter imeondoa ama imepunguza matangazo kwa baadhi ya watumiaji wake, watumiaji wachache ndio wanaopata nafasi hii ya kutumia huduma hii isiyo ya matangazo.
Vyanzo vingine vinasema ya kwamba wanaopata huduma hii kutoka Twitter ni watumiaji wachache ambao wamethibitishwa na pia wana wafuasi wengi… ila inaonekana pia sio kila aliyethibitishwa anaingia katika huduma hii wenyewe Twitter wakisema wanachoangalia ni akaunti iliyo ‘active’ zaidi, yaani inayotweet, yenye followers na ambayo inawasiliana na wengine zaidi.
Jambo la muhimu kukumbuka ukisoma makala hii ni kwamba Twitter imekuwa ikitegemea saana matangazo katika mtandao wake ili kujiendesha, ni kweli kwamba mapato yote ya twitter yanatoka katika matangazo. Mwaka 2015 ilikusanya karibu $bilioni 2 za kimarekani kutoka katika matangazo.
Pengine Twitter wanataka kufanya majaribio ya Twitter bila ya matangazo na pindi watakapo ona inakubalika wakaileta ila kwa kulipia kiasi fulani cha pesa kwa muda fulani, hii itakuwa kama vile ambayo Youtube wanafanya.
Kwa mujibu wa mtandao wa Redcode mpango huu ulianza wakati mkurugenzi mtendaji wa Twitter akiwa ana kaimu nafasi ambayo anaishikilia na inaonekana yeye anaiunga mkono huduma hii.
Kwa kuwa huduma hii wameanza kutumia watu wachache sana basi ni vigumu kujua hasa itakuwa na madhara gani katika mapato ya kampuni ambayo yanatokana na matangazo.
No Comment! Be the first one.