Kuna mengi tuu ambayo Twitter inapitia katika kipindi cha miezi kadhaa sasa kiasi kwamba hata aliyekuwa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Jack Dorsey kuamua kujiweka pembeni na kazi hiyo lakini hatua hiyo imekuja na mabadiliko ya kutoruhusu usambazaji wa picha/video za watu binafsi bila ya ruhusa zinazowahusu!
Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii ambayo inakabiliana kuja na mbinu mbalimbali ambazo zitawwafanya wasijikute mahali pabaya na mamlaka za kwenye nchi mbalimbali na hata Umoja wa Ulaya. Kuanzia Novemba, 30 2021 imezuia usambazaji wa picha ama picha mnato (video) zinahusu watu mbalimbali ya wao kukubali vitu hivyo vinaweza kusambazwa.

Katazo hilo lina sura mbili!
Katazo hilo la kutosambaza picha/video bila ya ruhusa haliwahusu watu mashuhuri iwapo vitu hivyo vitakwenda sambamba na maneno yanayohusu chapisho hilo iwapo litahusu kitu ambacho kina faida kwa watu. Hata hivyo, Twitter itaangalia kuangalia kile ambacho kinachapishwa kwenye mtandao huo wa kijamii ilikuwafanya wasijikute matatizoni.
Kwa watu binafsi (ambao sio mashuhuri) wanaweza kuomba Twitter waondoe chapisho ambalo linawahusu iwapo wataripoti kisha mtandao huo wa kijamii ukajiridhisha kuwa kilichoripotiwa kimekiuka sera walizoziweka.
Muda tuu Twitter walishaacha kuweka wazi taarifa binafsi kama namba ya simu, umri, anwani ya makazi lakini pia bado watu mbalimbali wananyoonyesha kidole mtandao huo wa kijamii kuhusu machapisho yanayohusu unyanyasaji kwa sababu ya rangi, jinsia, n.k.
Vyanzo: Gadgets 360, CNET
No Comment! Be the first one.