Kampuni ya Uber Technologies ya Marekani imetoa taarifa yake ya Uwazi kwa umma na kusema kwamba imeombwa na kutoa taarifa za watu milioni 12 ambao walitumia huduma hizo kwa Mamlaka na mashirika mbali mbali ya umma nchini Marekani.
Kampuni ya Uber ambayo imekuwa ikikuwa kwa kasi na kuitanua kwa kufungua matawi duniani kote ikiwamo Afrika imesema katika ripoti yake kwamba pamoja na kutoa taarifa za watu hao milioni 12 pia ilitoa taarifa za watu 469 kwa taasisi za sheria za selikari.
Ripoti hiyo inasema kwamba taarifa hizo zilitolewa kufuatia maombi ya juu ya taarifa za watumiaji hao kama vile ni wapi ambapo walishushwa, wapi walipochukuliwa na pia taarifa juu ya safari zao.
Hata hivyo maombi ya taarifa hizi hayakuwa kwaajiri ya kufanyia ujasusi ama kufatilia maisha ya watu bali mengi yalikuwa kwaajiri ya kuchunguza udanganyifu ama matumizi ya credit card ambazo zilipotea.
Makampuni mengi makubwa yanakwepa kutoa taarifa za watumiji wao kwa serikali kwasababu kufanya hivyo kuvunja faragha ya wateja wao. Hata hivyo watuwengi wameipokea kwa mtazamo chanya habari hii hasa ukizingatia taarifa hizi ziliombwa kwaajiri ya uchunguzi wa uhalifu.
Kampuni hiyo ipo njiani kuingia Tanzania.
Vyanzo: Reuters na pia mitandao mingine