Moja kati ya huduma za usafirishaji wa kukodisha ulijpiatia umaarufu kutokana na mambo mbalimbali hasa kwa dereva katika ufanisi wake wa kazi, Uber ni moja kati ya huduma hizo na kizuri zaidi nchini Tanzania Uber ipo na inasaidia sana.
Uber ni kampuni ambayo imekuwa ikikumbwa na misukosuko, kashfa mbalimbali, mabadiliko ya uongozi, n.k lakini kampuni hiyo imeweza kuendelea na biashara yake mpaka hivi leo na katika msimu huu wa sikukuu Uber waongeza vitu vipya kwenye programu tumishi ya Uber.
Mapya yaliyoongezwa kwenye app ya Uber.
Katika utoaji wa huduma ya usafirishaji una changamoto nyingi tu ambazo kila leo zinaibuka changamoto mpya lakini kwa Uber hata kama inatoa huduma ya usafirishaji lakini kwa derva yoyote aliyejiunga na Uber ana utofauti mkubwa sana na dereva mwingine yeyote na yule anayejishughulisha na biashara ileile wanayofanya Uber.
Uber ni nini? Uber ni huduma ya usafirishaji kwa kukodisha lakini anayekodiwa gari inakuwa ni ya kwake ikiwa na muonekano mzuri (sio mbovu), yenye vibali vyote. Dereva wa Uber hapangiwi hesabu yake kwa siku/wiki wala mwezi na dereva wa Uber anaitwa kutoa huduma kupitia kwenye app ya Uber/tovuti.
Usafiri wa Uber jijini Dar Es Salaam
Live Location. Kama ilivyo kwenye masasisho ya hivi karibuni kwenye WhatsApp kuhusiana na kipengele cha live locationvivyo hivyo Uber nao wameongeza kipengele hicho kwenye app yao jambo ambalo litawezesha kujua kwa urahisi alipo mteja/dereva wa Uber bila hata ya kumpigia simu kutaka kujua yupo wapi/amefika wapi.
Kipengele cha ‘Live location’ ambacho unaweza ukasambaza na dereva akajua mahali ulipo.
Uwepo wa alama maalum (Beacon) kwenye magari ya Uber kwa ajili ya kutambulika kiurahisi. Barabara zetu hasa za mijini zina magari mengi kitu ambacho kinaweza kusababisha mtu kutoweza kutambua kwa urahisi kuwa dereva wa Uber ameshafika kumpeleka anapohitaji ila kwa uwekekaji wa alama maalum kwenye magari ya Uber ni dhahiri gari la Uber litaweza kutambulika kwa urahisi.
Beacon-alama maalum ambayo Uber imeamua magari yake iwe nayo ili kuweza kutambulika kwa urahisi zaidi kwa aliyehitaji huduma yake.
Uwezo wa kumkodia mtu huduma ya Uber. Inawezekana ndugu, rafiki/jamaa anahitaji huduma ya Uber kwa wakati huo lakini labda hana simu janja karibu. Uber inamuwezesha yeyote mwenye app ya Uber kuweza kuita Uber kwa ajili ya mhitaji bila kujali sehemu alipo anayeitaji wa huduma ya Uber. Kujua zaidi kuhusu kuweza kumkodia mtu Uber BOFYA HAPA.
Kutumia mtu mwingine vocha (credit) kupitia kwenye app ya Uber. Kwenye app ya Uber kadri mtu anavyozidi kuitumia programu tumishi ya Uber ndivyo anavyozidi kupata vocha kutokana na matumizi yake, vocha ambazo pia mtu anaweza akamtumia mtu mwingine na akawa na uwezo wa kuzitumia. Jinsi ya kutuma vocha kwenye app ya Uber: Unafungua menyu kwenye Uber ya Uber>>Send a gift>>Select amount kisha mchague unayetaka kumtumia hizo vocha (credits) na weka ujumbe wowote kwenda kwa mpokeaji.
Kuna wale ambao wakiwa kwenye gari tu basi wanakuwa wagonjwa mathalani kutapika, kusikia kizunguzungu. Uber kupitia kwenye magari yake yanayojiendesha yenyewe inafanyia kazi kuwezesha magari hayo kuwa na uwezo wa kupunguza ugonjwa wa aliyekodi gari la Uber.
Gari inayojiendesha yenyewe kutoka Uber ikiwa na dereva wa akiba; kama ikipata tatizo na kushindwa kujiendesha basi dereva wa akiba aliendeshe.
Kwa kuweza kutambua na kujua kuwa mtu aliyekodi ana tatizo la ‘kuwa kama mgonjwa gari linapotembea’ hivyo kutumia mbinu kama kumtetemesha kwa kiasi fulani wakati gari hiyo inatembea huku akiwa amefunga mkanda, kumuwashia taa za kuvutia akiwa anasoma jarida/gazeti kwenye gari.
Umeshawahi kutumia huduma ya Uber? Na je, unadhani kwa maboresho hayo huduma ya Uber itaimarika mara dufu hasa katika msimu wa sikukuu?
Vyanzo: Gadgets 360, tovuti ya Uber, The Verge
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|