Katika Huawei P9 kampuni ya Huawei imefanikiwa kuja na sima janja ya kiwango cha juu sana – kuanzia kwenye teknolojia ya kamera, uwezo wa ndani na ata muonekano. Ubaya? – Tayari wengi wanaona simu hiyo imeiga ubunifu wa Apple na simu zake za iPhone.
Kuweka suala la kuiga muonekano wa sasa wa simu za iPhone bado simu ya Huawei P9 ni ya kisasa sana, ebu tuifahamu zaidi.
Sifa za Huawei P9
Huawei P9 inakuja katika matoleo mawili, kuna Huawei P9 Lite na Huawei P9 Plus. Huawei P9 Lite inaukubwa wa inchi 5.2 (resolution – 1920×1080)- LCD panel, huku Huawei P9 Plus inaukubwa wa inchi 5.5 (1920X1080) – AMOLED panel.
Toleo la P9 Lite linakuja na diski uhifadhi wa GB 32 (RAM GB 3) na GB 64 (RAM GB – 4), wakati P9 Plus inakuja na kiwango cha GB 64 (RAM GB 4).
Kiwango cha betri kwa Huawei P9 Lite ni mAh 3,000, wakati P9 Plus ni mAh 3,400.
Sifa zinginezo…..
- Teknolojia za mawasiliano: GSM/ HSPA/ LTE
- Laini ndogo ya Nano-SIM
- Ukubwa: Inchi 5.2 na 5.5
- Toleo la Android: Android 6.0 Marshmallow
- Ukubwa: Kuna ya GB 32 (RAM kiasi GB 3) na GB 64 (ram KIASI GB 4)
- Prosesa: Quad-core 2.5 GHz Cortex-A72 na quad-core 1.8 GHz Cortex-A53
- Kamera: Nyuma ina kamera kuu mbili kwa mpigo za MP 12, F/2.2, huku kamera ya selfi ikiwa ni ya MP 8 (f/2.4)
- Betri: Inatumia betri limejengewa ndani, halichomoki
Teknolojia ya kamera 2 kwenye simu ya Huawei P9
Ndio kabisa, Huawei katika P9 wamejizatiti katika kuweka ubora wa juu kabisa katika eneo la kamera. Kuna kamera mbili nyuma ya simu hii zenye uwezo mkubwa wa MP 12 huku zikitumika zote kwa wakati mmoja ili kuhakikisha picha inakuwa na ubora wa juu kabisa.
Tutegemee makampuni mengi mwaka huu na kuendelea kuja na teknolojia hii katika simu zao. Tayari kuna uvumi ya kwamba ata toleo lijalo la iPhone linaweza beba teknolojia hii, ila kwa sasa Huawei ndio wamefanikiwa kuileta katika ubora wake kabisa.
Shutuma za Kuiga ubunifu kutoka Apple
Apple ni moja ya kampuni iliyowekeza zaidi katika masuala la ubunifu wa bidhaa zake, hii ina maana saa nyingine wengi wanajikuta wakiiga vitu kutoka Apple na katika P9 shutuma kwa kampuni ya Huawei zimekuwa kubwa sana ya kwamba wameiga muonekano na teknolojia kutoka iPhone. Je Apple watawaburuza mahakamani? Kuna weza kukawa na hako kauwezekano.
Je hili lina ukweli? Tazama hizi picha na utuambie….
Teknolojia ya kutumia nati spesheli katika ufungaji wa simu za iPhone ulibuniwa na wao wenyewe – Apple. Na katika P9 inaonekana mfumo huo huo umetumika.
Bei na upatikanaji wake…
Simu ya Huawei P9 imetambulishwa rasmi mwezi wa nne…bei hizi kwa soko la Afrika Mashariki ni makisio yetu tuu kutokana na bei za simu hizo zilizotambulishwa rasmi Ulaya na tutaziupdate mara moja tukipata makisio ya bei rasmi.
Huawei P9 Lite
- GB 32 – Tsh 1,500,000/= | Ksh 68,500/=
- GB 64 – Tsh 1,620,000/= | Ksh 74,200/=
Huawei P9 Plus
- GB 64 – Tsh 1,870,000/= | Ksh 85,600/=
Huawei washafanikiwa kuwa moja ya watengenezaji wa simu wakubwa nyuma ya Samsung na Apple, na kupitia simu hii tunaona wanavyotaka kujitutumia katika kutoa simu janja za hadhi ya juu kushindana na iPhone na simu za familia ya Samsung Galaxy. Tuambie mtazamo wako wa simu hii, ubunifu wake na bei yake! 🙂
Imeandikwa kwa msaada wa WIRED.COM, na mitandao mbalimbali