Kampuni ya Infinix inafahamika kwa matoleo ya bei ya chini yenye kiwango kizuri cha ubora, na simu yao ya Infinix Smart 4 inadhihirisha hilo. Ni simu nzuri, hasa kwa bei ya chini yenye mfumo endeshi wa Android, betri nzuri na camera nzuri pia.

Simu hii iliingia sokoni rasmi tarehe Oktoba 2019.
Sifa za simu hii ni kama;
- Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inchi 6.6
- Prosesa ya Mediatek MT6761 Helio A22
- Mfumo endeshi wa Android 9.0 uliorahisishwa (Go Edition).
- RAM ya GB 1 na diski uhifadhi ya GB 16, na pia kuna toleo la GB 64
- Kamera ya nyuma yenye megapixel 8 kwa toleo la GB 16, megapixel 13 kwa toleo la GB 64 na kamera ya mbele/selfi yenye megapixel 5.
- Betri yenye uwezo wa 4000 mAh
Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G, pia Bluetooth na WiFi. Ina teknolojia ya usalama ya alama za vidole (fingerprint). Inakuja na uwezo wa kusikilia redio katika mfumo wa FM.
Ina sehemu ya kuchomeka earphones na sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0 . Ina matoleo matatu ya rangi, Nyeusi (Midnight Black), Samawati (Quetzal Cyan) na Zambarau (Cosmic Purple).
Bei: Kwa wastani wa Tsh 200,000 kwa toleo la GB 16, na 230,000 – 240,000 kwa toleo la GB 64.
No Comment! Be the first one.