Teknolojia ya magari inayoonekana kuja kwa kasi sana katika nchi zilizo katika dunia ya kwanza ni dhahiri kuwa magari hayo yamekuwa mbadala wa nguvu kazi kwani haihitaji uwepo wa dereva ili kuweza kufika safari yake.
Udukuzi katika magari yanayojendesha yenyewe ni jambo ambalo makampuni yanaunda magari hayo yamekuwa yakiangalia jambo hilo kwa ukaribu sana ili kuwezesha magari hayo kutopata ajali ukizingatia uwepo wa dereva ndani ya gari si wa lazima sana.
Kilichogundulika kuhusu udhaifu wa kwenye magari yanajiendesha yenyewe.
TImu ya watafiti kutoka vyuo vikuu vinne tofauti huko Marekani wamebainisha jinsi gani gari linavyoweza kutafsiri sivyo ndivyo alama za barabarani madhalani alama inayoonyesha gari linatakiwa kusimama lakini gari linalojiendesha lenyewe likatafsiri alama hiyo kama alama inayotaka gari hilo litembee mwendo 45mph.

Ipo mifano mingi tu inayoweza kudhihirisha kosa/makosa ambayo yanaweza kufanywa na gari lisiloendeshwa na dereva na kikubwa katika kudhihirisha kuwa magari yanayojiendesha yenyewe yana udhaifu uliobainika timu ya watafiti ilihitaji kuingia kwenye mtambo wa kamera na ule ambabao unaohusika kutafsiri rangi/alama za barabarani.

Tesla kwenye magari ya Model S yanayojiendesha lenyewe (toleo la hivi karibuni) yamewekwa kifaa maalumu cha kuweza kusoma na kutambua alama za barabarani ingawa bado hazijaamriwa nini cha kufanya iwapo alama husika ikitambulika vinginevyo na ile inayotambulika kwenye kompyuta.
Zipo kampuni mbalimbali ambazo zimetengeneza vitu vya kufafishia kioo cha gari (wipers) ambazo ni ndogo zitakazoweza kutoa uchafu wowote hata liwe ni doa dogo sana kwenye kioo.
Tayari Uingereza imetoa waraka maalum wa jinsi gani magari yanayojiendesha yenyewe yanavyotakiwa kuwa ili kuepukana na wizi/udanganyifu wa aina yoyote.
Vyanzo: Fortune, Telegraph