Serikali ya Uingereza imetishia kufungia mitandao ya kijamii kupitia kampuni zao ikiwa hazitatoa jumbe ambazo zinazoweza kuwa hatari kiafya.
Waziri wa Afya Uingereza, Bw. Andrew Marr ameeleza kuwa kampuni hizo zisipokufuata maagizo ya serikali, sheria itapitishwa kuzipiga marufuku na pengine hata itungwe sheria itakayowezesha jambo hilo kuwa na nguvu zaidi.
Lengo la serikali ya Uingereza ni kushirikiana na makampuni yanayomiliki mitandao ya kijamii kuweza kuondoa jumbe ambazo zinaweza kusababisha watu kujiumiza/kujiua.
Msichana Molly Russel wa miaka 14 alijitoa uhai mnamo 2017 baada ya kutazama ujumbe uliomsumbua kuhusu kujiua. Baba yake mtoto huyo alieleza kuwa anaamini mtandao wa Instagram, chapisho kwenye Pinterest vilichangia mwanae kujiua.