Wakati yamebakia masaa machache simu mpya za iPhone 5S and 5C kuingia sokoni hizi ni baadhi ya picha za raia mbalimbali huko London na Manhattan, Marekani waliojitokeza siku kadhaa wakisubiri duka kufunguliwa nao wawe wa kwanza kabisa kununua simu hiyo.
Je wewe unaweza ukawa na mapenzi ya namna hii ya kuacha shughuli zako na kuweka kambi hadi upate kitu kama hichi? tena si bure 🙂 ?
Shabiki wa iPhone akiwa nje ya duka la Apple jijini London |
Makazi mengine jijini London nje ya Duka la Apple |
Ingawa kuna baridi kali lakini halikuweza kuwazuia watu kulala katika kambi hizo |
Na huko nchini Marekani hali ni kama hii |
Wakati iPhone 5S na iPhone 5C zinaingia sokoni masaa machache yajayo mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS 7 tayari ushaanza kupatikana kupitia iTunes kwa watu wenye toleo la iPhone 4 na zaidi, iPad 2 na zaidi, iPad Mini na iPod Touch 5.
Ila hatukushauri kuhamia kwenye iOS 7 kwa sasa, kwani kuna malamiko ya apps nyingi kutofanya vizuri baada ya kuhamia(upgrade) iOS 7. Na utakapoamua kuhamia programu hii hakikisha ume’back up’ vitu vyako kupitia iTunes.
Bei ya chini kabisa ya iPhone 5S inatauzwa takribani Tsh 1,046,837/= wakati iPhone 5C itakuwa takribani Tsh 885,537/=.
No Comment! Be the first one.