Tunatumia simu, kompyuta, memori za ziada, n.k lakini vitu vyote hivyo zipo vina ukubwa wa ambao ukitathmiini ni namba shufwa tu ndio zinakuwa zimebeba kifaa husika.
Kila swali lina jibu au majibu kulingana na mada/kipengele husika na pengine wewe ni kati yale ambao wakati fulani walishawahi kujiuliza “Kwanini simu, memori ya ziada, kompyuta ukiangalia ukubwa wake upo kwenye kundi la namba shufwa?”. Jibu lipo tena lakini ni muhimu kukumbushana kidogo.
Namba shufwa ni namba yoyote inayogwanyika kwa mbili (2) bila kubaki. Hapa ndio utavuta taswira kuwa vifaa vyetu vya kidijiti (vilivyo na uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu) ukubwa ambao umbo kwenye kundi hilo la namba; GB 8, GB 16, GB 32 na kuendelea.
Memori za ziada zenye ukubwa tofauti tofauti.
Ukweli kuhusu namba shufwa kwenye vifaa vya kutunza kumbukumbu.
Kompyuta, rununu, kifaa cha kidijiti vinatafsiri chochote katika ufanyaji wake wa kazi ni mfumo wa sifuri na moja (0/1) ikimaanisha2^n (n=namba yoyote nzima kuanzia sifuri). Sasa basi kwenye kwa sababu namba zilizokamilika zipo zinambulika kama 0/1 basi hesabu kamili inaweza kuwa kama ifuatavyo:-
Sasa kama kifaa husika kina ukubwa wa GB 128 hiyo inakuwa ni sawa na kama inavyoonekana pichani.
Tafsiri ya ukubwa wa 128 kwenye vifaa vya kidijitali.
Hivyo basi kutokana kifaa ambacho kinaweza kusoma kitunza kumbukumu kinafasiri mambo katika mfumo wa 0/1 ambao upo juu ya mbili ndio maana daima jibu litapatikana katika namba shufwa.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|