Ukikutana na mlemavu wa macho ambae hataki kuona kama ulemavu wake ni kikwazo au kutoamini kuwa matumizi ya simu rununu ni kikwzo kake basi utapenda uone jinsi anavyoitumia simu hiyo.
Kila kiungo katika mwili wa binadamu kina umuhimu wake lakini binafsi naona macho ni mlango wa fahamu muhimu sana katika maisha ya kila siku. Kama umeshawahi kumuona mlemavu wa macho akiwa anatumia simu janja nina amini ulitaka kumuuliza/ulimuuliza swali hili: “Unawezaje kutumia simu rununu wakati huna uwezo wa kuona?” lakini pengine hakukujibu kutokana na sababu mbalimbali.
Teknolojia kwa watu wenye ulemavu wa macho.
Kutokana na kutokuwa na uwoni basi sauti ndio mwongozo kwa yeyote yule ambae ana huoni hafifu au haoni kabisa. Kwenye simu janja nyingi za kisasa ukingia Settings>>Accessibility>>TalkBack hapo ndio mkombozi kwa yule asiyeona.
Kipengele cha TalkBack kinatoa mwongozo/maelezo katika mfumo wa sauti kwa kitufe chochote kile ambacho mtu atabonyeza na hivyo kujua ni wapi alipobonyeza; kutumia kipengele hiki kinahitaji usikivu na uelewa wa kiasi cha kuridhisha wa lugha ya Kiingereza.
Kwenye iPhone kipengele sawa na TalkBack kinaitwa VoiceOver ambapo chimbuko lake ni baada ya mlemavu wa macho kuuliza “Kama simu za mguso ndio teknolojia ya baadae sisi tusioona tutaendelea kuwa gizani?“. Miezi 6 baadae Apple ilitoa masasisho ya programu endeshi na ikajumuisha kipengele cha VoiceOver.
Nikiwa kama mtu ambae nimeshashuhudia nathubutu kusema mlemavu wa macho anaweza akafanya kazi zake vizuri kabisa bila usaidizi na akafanya pengine vizuri zaidi kuliko hata yule ambae ana uwezo wa kuona.
Teknolojia bado inakwenda mbali na kuna programu inafanyiwa kazi ambayo kazi yake ni kutafsiri picha katika mfumo wa sauti ili kumpa picha halisi kichwani mwake mtu asiyeona kuhusu kile kinachoonekana.
Vyanzo: Mawazo binafsi, Insider