Sababu iliyokuwa inatolewa na kampuni ya Smile Communications muda mrefu juu ya bei zao za vifurushi vya intaneti inaonekana ndiyo sababu hiyo hiyo kampuni ya Tigo itabidi kutumia kueleza wateja wake waliopata furaha kubwa baada ya kusikia ujio wa teknolojia ya 4G kwenye mtandao huo.
Soma Pia – Tigo na 4G: Smile Yapata Ushindani! Je tupo tayari kwa 4G?
Sababu kuu ambayo imekuwa inatolewa na mtandao wa Smile katika eneo la gharama za vifurushi vyake ni kwamba inagharimu pesa nyingi sana kuweka mitambo ya 4G, kuisimamia na kuiendesha. Na kutokana na sababu hii ndiyo maana bei zake ni ghari sana.
Kwa sasa mtandao wa Tigo unapatikana katika 4G katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam – Masaki, Oysterbay, Msasani, Mlimani City na Survey.
Bei ya vifusuhi vya 4G kwa mtandao wa Tigo ni kama ifuatavyo
- Siku 7 – GB 1 – Tsh 10,000/=
- Siku 7 – GB 3 – Tsh 25,000/=
- Siku 30 – GB 5 – Tsh 40,000/=
- Siku 30 – GB 10 – Tsh 80,000/=
- Siku 30 – GB 20 – Tsh 150,000/=
Vifurushi vya Smile vyote vimepangiliwa kuwa vya siku 30 na ni kama ifuatavyo;
- Siku 30 – GB 1 – tSH 17,500/=
- Siku 30 – GB 5 – Tsh 42,500/=
- Siku 30 – GB 10 – Tsh 80,000/= (Pia wana kifurushi kwa ajili ya matumizi makubwa jioni na wikiendi, wakati mwingine wa siku unaruhusiwa kutembelea mitandao kama ya kijamii, barua pepe, nk ila si mitandao mizito kama vile YouTube – Kwa GB 10 utalipita kwa Tsh 69, 000/=)
- Siku 30 – GB 20 – Tsh 155,000/=
Smile wana vifurushi vingine zaidi lakini nimeviweka vichache tuu ili kukupa picha ya tofauti za kibei kati ya zile za Tigo. Faida kubwa kwa Smile ni kwamba wanapatikana sehemu kubwa ya jiji la Dar es Salaam na hivyo mkazi wa jijini hana wasiwasi wa eneo atakaloenda wakati kwa Tigo bado maeneo wanayopatikana ni machache mno. Tigo pia wameweza kuchomeka vifurushi vyenye mvuto na kwa bei nafuu kidogo ukilinganisha na vya Smile, ila kwa watumiaji wakubwa basi bado wataona bora kutumia Smile.
Wengi tulifurahia kwa sana tukitegemea ushindani mpya wa Tigo katika huduma ya 4G italeta unafuu wa kibei lakini tunachoona ni kwamba bado, tofauti ni ndogo sana na haileti unafuu wowote katika kupata teknolojia hii ya kisasa.
Soma Pia – Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k
Tungependa kusikia kutoka kwako, tuambie maoni yako kupitia eneo hapa chini.
No Comment! Be the first one.