Mawasiliano kwa njia ya barua pepe ni jambo ambalo limezoeleka na kutumiwa na wengi kasi cha kwamba kuamnika kutokana na uharaka wa kupata majibu kuhusiana na kile ulichowasiliana na mtu kwa barua pepe.
Jambo la mtu mwingine kutumia barua pepe yako bila ya wewe kujua kwa njia ya udukuzi au mtu ameweza kujua nywila yako basi baada tu ya kumpa kisogo akaanza kuitumia pasipo ya wewe kujua jambo linaloweza kusababisha watu kuhamaki kutokana na jumbe watazokuwa wakizipata kwa njia ya barua pepe kutoka kwako.
“Namna gani mtu anaweza kuwa salama dhidi ya udukuzi wa barua pepe?” ni swali ambalo limekuwa likisumbua wengi lakini leo TeknoKona tutakupa elimu ya jinsi ambavyo unaweza kufanya barua pepe yako iwe ni vigumu kudukuliwa:
- Kuangalia “Settings” za barua pepe yako (Gmail). Inawezekana kabisa mtu akawa anasoma na hata kujibu jumbe zako zilizotumwa kwa njia ya barua pepe bila ya hata wewe mhusika kugundua kama ujumba/jumbe hizo zimeshasomwa na mtu mwingine. Je, jambo hilo linawezekanaje? Ni hivi, Settings>>Accounts and Import>>Add an email account>>Forwarding and POP/IMAP (hapo mtu anaweza akaweka barua pepe yake na akawa anapata jumbe zako zote na hata pia kuweza kujibu jumbe hizo).
Kwa kutumia “Forward email address” unaweza ukaweka barua pepe yako nyingine na kuweza kujibu jumbe ulizotumiwa bila hata ya kuingia kwenye akaunti yako ya Gmail. - Badilisha nywila yako mara kwa mara. Matumizi ya nywila katika mambo mbalimbali yamekuwa katika mstari wa mbele lakini suala si tu kubadilisha nywila mara kwa mara lakini cha msingi na cha kuzingatia ni kuhakikisha unatengeneza nywila ambayo itakuwa ni ngumu kubashirika (Settings>>Accounts and Import>>Change password). Kujua mengi zaidi kuhusu nywila INGIA HAPA.
Ni muhimu kuweka nywila iliyo madhubuti kuzuia udukuzi dhidi ya kile unachojaribu kukificha. - Kuwa na ulinzi “Mara mbili mbili”. Kwa namna moja au nyingine mtu aweza akajua nywila unayotumia kuingia kwenye barua pepe yako jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa akaunti yako ya barua pepe. Kwa kuliona hilo na kuendana na kasi ya utandawazi Gmail, Facebook, n.k wamewezesha kuweka ulinzi wa akaunti yako zaidi tu ya kuwa na nywila (two-step verification). Hii ina maana ya kwamba kabla tu ya kuingia kwenye akaunti yako kuna tarakimu maalum zitakazotumwa na Goofle ambazo utapaswa kuzingiiza ili kuweza kuwenda kwenye akaunti yako (Gmail, Facebook, n.k).
Kwa usaidizi huu ni dhahiri kuwa mtu hatoweza kuingia kwenye akaunti yako bila kuingiza tarakimu hizo mahususi ambazo zitahitajika ili mtu kuweza kuingia kwenye akaunti yako na zinabadilikabadilika.
Soma pia: Maujanja/Mbinu mbalimbali za kwenye simu/kompyuta au intaneti
- Kuweza kuipata akaunti yako. Inaweza kutokea ukashindwa kuingia kwenye akaunti yako ya Gmail kutokana na kusahau nywila/akaunti yako kudukuliwa. Hali hiyo ikitokea haimaanishi kuwa hutoweza kutumia akaunti yako, unaweza ukarudissha akaunti yako kwa kuandika barua pepe ambayo unaweza ukaingia na kufuata maelekezo ili uweze kurudisha akaunti yako.
Katika ule mchakato wa kurudisha akaunti yako kuna maswali kadha wa kadha kama namba yako ya simu, ulifungua lini akaunti yako ya Gmail (siku ya kwanza kutengeneza akaunti yako), n.k ni baadhi tu ya maswali ambayo kama utayajibu kifasaha kulingana na rekodi walionayo Google basi utatumiwa ujumbe kwenye ile akaunti yako nyingine na kisha utafuta maelekezo yatakayofuata.
Ni muhimu sana kuhakikisha unatunza taarifa zako za mitadaoni katika ulinzi wa hali ya juu ukizingatia njia mbalimbali tulizoziainisha hapo juu. Jisikie huru kusambaza makala hii ili na wengine wapate kuelimika.
Vyanzo: The Guardian, mawazo binafsi.
3 Comments
Comments are closed.