Inafika wakati unajiuliza ni laptop gani ununue kwa ajili ya shule, ofisi au nyumbani. Yapo mambo muhimu ya kuangalia, yani, ukubwa, kasi ya kufanya kazi (‘processor’), ukubwa wa kumbukumbu yake (‘RAM’) na uwezo wa kukaa na chaji, ila siku zinavyozidi kuenda, mambo kama shepu na uzito wa kompyuta yanaanza kupewa umuhimu wake na ndio maana Apple waliamua mapema kutoka na MacBook. Muda haukupita sana na Intel nao, wakajibu mapigo hayo kwa kutoka na ‘Utrabooks’ amabazo tulizitambulisha vyema hapa. Kama wewe ni mtu wa ofisini, shuleni au mtu wa mishemishe nyingi, hii makala itakufaa sana na kuna nafasi kubwa utatamaani kununua kompyuta hizi.
MacBook na Ultrabooks ni laptopu nyembamba, nyepesi na zenye uwezo mkubwa. Laptopu hizi zimetengenezwa kukusaidia usichoke kirahisi wakati unasukuma gurudumu la taifa kwa mihangaiko ya hapa na pale. Octoba hii, teknokona tunakuletea orodha ya laptopu hizi bomba za kuzingatia ukiingia sokoni.
Yoga Pro 2 ni laptopu mpya zaidi kutoka kwa Lenovo, kampuni ya China ambayo ilinunua sekta ya kompyuta za watu binafsi kutoka kwa IBM. Ultrabook ya Yoga inakupa u-potabo, huku ikiwa imejazwa chaguzo kibao kwa bei nafuu.
Yoga inasifiwa kwa uwezo wa kukunjika unavyoitaka, yani, unaweza ukaikunja uitumie kama laptopu ya kawaida au ukaisimamisha kama laptopu ya mguso (‘touch-screen stand’) au unaweza kuikunja kabisa ukaibeba kama tableti.
Lenovo wanajivunia pia uwezo mkubwa wa betri ya Yoga. Laptopu hii inaweza kukaa na chaji mpaka masaa 9, kitu ambacho ni habari njema sana kwa wafanyakazi wenye mizunguko ya muda mrefu. Unaweza kuichagua Yoga yako katika rangi kadhaa na utafaidika kwa kibodi inayowaka taa. Wachambuzi na wachangiaji wa mtandao wa LifeHacker wameisifia Yoga kwa kuwa na skrini inayovutia, kubebeka kirahisi na kudumu ukilinganisha na bei utakayooilipia.
Angalia Lenovo Yoga Pro 2 mtandaoni: Lenovo IdeaPad Yoga 2 Pro na video
Sifa zake:
Mfumo-endeshaji – Windows 8, 8.1
Prosesa – Intel Core i7 au Core i3 processor, 4th Generation Intel Core i3-4030U processor (1.90GHz 1600 MHz 3MB)
Skrini – QHD+ LED (3200px x 1800px) display on a 13.3″ Glossy Multi-touch IPS display
Masuala ya ‘Graphics’ – Integrated Intel HD 4400
Kumbukumbu 8GB RAM, 1600.0 MHz.
Uhifadhi -Hadi 512GB SSD
Mtandao Wayalesi; 802.11b, 802.11g, 802.11n.
Betri – Kati ya masaa 8 na 9 kwa kuchaji mara moja
Bei $1000 na zaidi
Ukubwa:Inchi 13×8.7×0.6
1.36 Kg
Mambo mseto; Kamera, Kibodi iliyomulikwa, Bluetooth Version 4.0, Mini HDMI, Microphone, SD card
2.ASUS’s Zenbook Prime
Ultrabook za Zenbook Prime zinasifika kwa skrini yenye muonekana unaovutia na zimetengenezwa kudumu. Mbali na dizaini yake, Ultrabook hizi inasifika zaidi kwa uwezo wa kuhimili mifumo-endeshaji mingine zaidi ya Windows. Zenbooks zinahimili linux vizuri, ambayo ingawa inatumika na watu wachache ni muhimu pia. Unaweza kuchagua prosesa unayotaka na Zenbook na pia utafurahia skrini ya mguso, kibodi inayowaka na uhifadhi wa kutosha. Laptopu hizi zinakuja na chaguzo mseto kama ‘Intel WiDi’ inayokupa uwezo wa kutuma video unazotaka kwenda kwenye TV yenye teknolojia ya wayalesi.
Angalia Ultrabook za ASUS Zendbook Prime kwenye mtandao na video
Sifa zake:
3.Thinkpad X1 Carbon
Thinkpad ni Ultrabook inayosifika kikazi zaidi lakini watengenezaji wenyewe wanasisistiza kuwa zimetengenezwa kwa ajili ya watu wote. Hii ni Ultrabook nyingine kutoka kwa Lenovo, inayoendeleza jina na kibodi yenye ‘trackpad’ zilizokuwa kwenye kompyuta IBM amabao ndiyo watengenezaji wa zamani wa familia ya kompyuta za Thinkpad. Lenovo wameyaendeleza haya kwa sababu bado muundo wa kibodi na jina la Thinkpad bado linaamika na lina mashabiki wengi duniani. Ultrabook hii ngumu sana, ukizingatia inatengenezwa kwa matirio ya ‘Carbon-fibre’ ambayo ni nyepesi pia. Japo Thinkpad X1 ni ghari sana, imejazwa teknolojia ya hali ya juu na ugumu wake pia unaiweka kwenye chati.

Angalia Thinkpad X1 Carbon kwenye Mtandao na Video.
Sifa zake:
Mambo mseto: Biometrics kwa ajili ya ku-‘scan’ kidole chako kama passiwedi, RapidCharge Battery – 80% ya chaji ndani ya saa moja, Face-tracking technology, Spill-resistant keyboard.

4. Samsung Series 9 laptops
Sifa kuu za ultrabook za Samsung Series 9 ni skrini ya mguso, uwembaba, na uwezo wa kaufanya mambo ya kila siku bila wasiwasi. Laptopu za Series 9 zina bei ya juu, kuanzia dola 1300, kutegemea na mambo yaliyo ndani ya kompyuta hiyo. Zinasifika na wengi kwa uzuri na uwepo wa ‘matte screen’’ ambayo inapunguza mwanga wa jua au taa kung’aa kwenye skrini, kitu ambacho kinaumiza macho. Modeli inayosifika zaidi kutokana na maoni ya watu wengi katika familia ya Series 9 ni NP900X3C.Angalia Samsung Series 9 NP900X3C mtandaoni na kwenye video.
Sifa zake:
5. MacBook Air
MacBook Air siyo ultrabook, ila ipo hapa kama laptopu ya kwanza kabisa kama hizi. Ultrabook zilizuka baada ya mafanikio ya MacBook. Laptopu hii inatengenezwa kwa kampuni ya Apple Inc na unaweza kuiita muasisi wa laptopu nyepesi na nyembamba.

MacBook zinatengenezwa kwa chuma cha alumini. Inakaa na chaji kwa muda mrefu sana na inakuja na mfumo-endeshaji wa MAC OS X. Hadi sasa, Macbook haina teknolojia ya mguso wala MAC OS X haina uwezo wa mguso ila inasifika kwa dizaini ya kuvutia, skrini yenye muonekano mzuri kwenye giza na kioo ng’aavu (glossy-screen) na kibodi inayowaka gizani.
Angalia Macbook Air mtandaoni na video.
Sifa zake:

Hizi ndizo Ultrabook tano zinazosifika sana sokoni. Kama uko mbioni kununua mashine yako mpya, si mbaya ukajipima na kuzingatia hizi kabla kununua mwaka huu. Makala hii imezingatia uchambuzi na maoni ya watu mbalimbali kwenye mtandao wa LifeHacker na mitandao mingine kwenye intaneti. Mbali na laptopu hizi zilizotajwa hapa, pia kuna Ultrabook chache za kuzipa wazo pia kama kama Acer Aspire S7-392, inayosifiwa kuwa bora zaidi kwenye mtandao wa The Wirecutter. Uzuri wake ni pamoja betri inayodumu masaa mengi, dizaini ya kuvutia na bei nafuu, pamoja na mambo mengine ya ziada unayoweza ukayaongezea juu ya mashine kutoka kiwandani. Pia, kwa wale mashabiki nguli wa MIcrosoft, kuna Surface Pro 3 ambayo ipo juu sana kwa uwezo wake wa kuhimili mguso na Windows 8 na 8.1 kwa sababu imetoka kwao Microsoft wenyewe. Toshiba nao hawako nyuma. Unaweza ukaingalia pia Toshiba Satellite U845t. Laptopu hii haina mbwembwe nyingi ila wengi wanaweza kuvutiwa zaidi na bei yake ambayo iko chini zaidi ya ultrabook nyingine kwa kuuzwa kuanzia $799.
*Bei zote zilizotajwa hapa ni za ughaibuni kutoka kwa watengenezaji wenyewe. Kutumia bei hizo unaweza kukadiria bei za maduka ya kitanzania.
Picha na:
www.amazon.com, www.macworld.com, www.techland.com.vn, http://store.apple.com/us/buy-mac/macbook-air, www.loadthegame.com, www.speckproducts.com, www.pcworld.com, prohardver.hu, www.johnpopes.com, www.techradar.com, www.hdwallpapersphoto.com, okwave.jp, arstechnica.com, notebookspec.com, www.pcworld.com, www.engadget.com, www.gentechpc.com,www.etrubka.com.
Naomba kujua nitapata wapi Lenovo Yoga tablet 8, hapa dar es salaam ?