Unsane ni filamu tamu inayohusu mdada anayedhania amefungiwa kwenye hospitali ya watu wenye ugonjwa wa akili – waliodata, nje ya uamuzi wake. Muvi hii tamu imeongozwa na muongozaji filamu maarufu duniani, Steven Soderbergh.
Steven Soderbergh ameongoza filamu zingine maarufu kama vile muongozo wa filamu za Ocean’s (Ocean Eleven, na zinginezo), Magic Mike, na tamthilia ya Gray’s Anatomy.
Unsane si muvi ya kwanza kurekodiwa kwa kutumia simu, muvi ya kwanza ilikuwa inaitwa Olive – ambayo ilirekodiwa kwa kutumia simu ya Nokia N8. Pia kuna nyingine inaitwa Sundance na hii ilishinda hadi tuzo, hii ilirekodiwa kwa kutumia iPhone 5S mwaka 2015.
Kutokana na utumiaji wa simu tuu basi inasemekana maeneo mengi ya nje muvi hiyo ilirekodiwa bila ata ya wapita njia kugundua ya kwamba kulikuwa na muvi inayorekodiwa.
Tazama trela la muvi hiyo inayotegemea kuingia kwenye majengo ya sinema mwezi wa tatu mwaka huu, 2018.