Serikali ya Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuhusika na shambulizi la mtandaoni la Ijumaa kwenye tovuti zake. Takriban tovuti 70 za serikali zilizimwa kwa muda, katika shambulio hilo kubwa dhidi ya Ukraine katika kipindi cha miaka minne. Kabla ya tovuti kuzimiwa mtandao, ujumbe ulionekana kuwaonya Waukraine “kujitayarisha kwa mabaya”. Ambapo tovuti nyingi zilirejeshwa ndani ya masaa machache.
Marekani na Nato wamelaani shambulizi hilo na wametoa msaada kwa Ukraine. Urusi haijatoa maoni yoyote kuhusu udukuzi huo. Wataalamu katika wizara ya habari ya Ukraine walichapisha ratiba ya jinsi habari za shambulio hilo zilivyoenea, wakisema kwamba vyombo vya habari vya Urusi viliripoti kabla ya vyombo vya habari vya Ukraine.
Walidai kuwa mashambulizi hayo yalitokana na kile walichokiita kushindwa kwa Urusi katika mazungumzo yake ya hivi majuzi na Nato kuhusu Ukraine. Ukraine imekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa majirani zake, kwa kuwa na wanajeshi 100,000 wa Urusi karibu na mipaka yake. Huduma ya usalama ya SBU ya Ukrainia inasema katika muda wa miezi tisa tu mwaka jana “ilizuia” mashambulizi au matukio 1,200 ya mtandaoni.
Nato ilisema hivi karibuni itatia saini ya makubaliano na Ukraine kuhusu ushirikiano ulioimarishwa wa mtandao. Ikulu ya White House inasema kuwa itaipatia Ukraine msaada wowote inaohitaji kujikwamua kutokana na shambulio hilo. Mwanzoni mwa shambulio la Ijumaa, ujumbe kwenye tovuti zilizodukuliwa uliwekwa katika lugha tatu, Kiukreni, Kirusi na Kipolandi.
Miongoni mwa tovuti zilizolengwa ni tovuti ya Diia, mfumo muhimu unaojumuisha huduma za serikali ambazo huhifadhi data na vyeti vya chanjo ya kibinafsi. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, alisema rasilimali zake zote zinakusanywa ili kuisaidia Ukraine kukabiliana na “aina hii ya mashambulizi ya mtandaoni”.
Wakati ulimwengu umetazama kwa hofu kuongezeka kwa wanajeshi wa Urusi, jumuiya ya usalama mtandao imekuwa ikitazama na kusubiri aina fulani ya uvamizi wa mtandao.
Chanzo: BBC Tech
No Comment! Be the first one.