Mtandao wa WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii maarufu kabisa katika swala zima la mazungumzo ya papo kwa papo.
Licha ya WhatsApp kuwa na namba kubwa ya watumiaji na umaarufu uliokithiri, mtandao huo bado unahakikisha kuwa unawaletea watumiaji wake huduma nzuri.
Kwa sasa ili uweze kutumia mtandao huo ni lazima uwe umejiunga kwa kutumia namba yako ya simu katika mtandao huo.
Na namba yako ya simu ndio itakayaosababisha wengine waweze kukuona na kuanzisha mazungumzo na wewe ndani ya mtandao wa WhatsApp.
Vipi kama hili lingekua sio la ulazima? Yaani si lazima mtu awe na namba yako ya simu ili kuweza kuwasiliana na wewe ndani ya mtandao huu?
Hili sio jambo jipya kwa baadhi ya mitandao kama vile Telegram, ambapo kipengele hiki kinapatikana vizuri kabisa.
Kumbuka hiki ni kipengele ambacho kinatarajiwa kufika hivi karibuni kwa watumiaji wa mtandao huo wa WhatsApp.
Uzuri wa kipengele hiki ni kwamba kina manuufaa sana hasa kwa wale watu ambao hawapendelei namba zao za simu kusambaa katika mtandao huu.
Kinachofanyika ni kwamba watu wataweza kuchagua Username ambazo watakua wanatumia wao tuu na kasha namba zao zitakuwepo pale pale ndani ya mtandao huu lakini zitakua zimejificha (kwa siri/hazionekani kwa mtu mwingine)
Uzuri mwingine wa hiki kipengele ni kwamba utakuwa na uwanja mkubwa wa kuwasiliana na akaunti yeyote iwe ya binasfi au hata ya biashara ilimradi tuu ujue Username yake.
Swala la ulinzi na usalama ndani ya makundi limepewa kipaumbele kikubwa sana maana kama namba zako za simu zitakua zimefichwa (kwa usiri) maana wengine watakua na uwezo wa kuona username yako tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani hili litaleta mapinduzi kiasi gani katika mtandao huu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.