Kwanza Google (ALPHABET) wamiliki wa mtandao namba moja duniani kwa masuala ya video yaani YouTube. Wamefungua Biashara nyingine ya kujitegemea inayohusisha Muziki yaani YouTube Music. YouTube music bado ni changa sana katika sekta ya muziki kulinganisha na wenzake kama Spotify na Tidal na zingine
Kuna kipindi spotify ilikua ikiongoza kuwa ya kwanza katika ya huduma za muziki mtandaoni na pia nahisi mpaka sasa bado ni namba moja kwa sijaona ya kuipita. Sasa hivi makampuni mengi sana yamejiingiza katika kuleta huduma ya muziki kwa wateja wake mfano sasa kuna Apple Music, Pandoran. n.k
Tukirudi kwa Google Music, Je itaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuhakikisha inabaki kuwa juu??
Youtube Music App ambayo ni Bure lakini yenye matangazo, au unaweza lipia kiasi cha dola 9.99 kila mwezi ili kuepukana na matangazo hayo ambayo inakuruhusu kusikiliza miziki katika simu yako huku ukifanya mambo (Apps) mengine katika simu. Ambayo pia ina miziki mingi kuliko huduma nyingine yeyote kama hii. Kwanza kabisa Youtube Music ina miziki mipya mingi na pia wana madili makubwa na rekodi lebo kibao hata yale yanayohusu album kwa ujumla, show mbali mbali, muonekano wa wasanii katika vipindi mbalimbali katika Tv .n.k. Sasa hili tuu linatosha kuonyesha kwamba YouTube Music itakua kwa kiasi kikubwa kulinganisha na huduma hizo zingine kwani ina vitu au huduma ambazo wengine hawana
Ila Google wakitaka huduma yao (YouTube Music) izidi pasua anga inabidi wawekeze nguvu nyingi katika huduma hiyo. Vile vile kumbuka Google ndio mtandao namba moja duniani kwa lengo la kukusaidia kutafuta (Search) vitu mbalimbali katika mtandao. pia wanaweza tumia hii (google serach) kuhakikisha wanawafikia watu wengi zaidi
Apple Music Ilitoka Mwezi juni mwaka huu (2015) na mpaka sasa bado inahaha kutafuta watu wa kutumia huduma hiyo. Si maanishi kuwa haina watu, bali ina watumiaji wachache sana. Hapo mwanzo waliweza kupata watumiaji milioni 15 ambao walijiunga katika mtandao huo kwa lengo la kuujaribu (trial) baada ya muda watumiaji milioni 6.5 tuu ndio waliokubali kulipia na kuendelea kutumia huduma hiyo. Hii inaonyesha ni jinsi kadi kuendesha huduma hii kulivyo kugumu
SOMA PIA: Google waleta App Spesheli Kwa Music: YouTube Music
Lakini Google wana njia zake bwana. Kwa mfano Google iliachia App yake kwa ajili ya picha mwezi mei mwaka huu (2015) na App hiyo ni ya bure kule sokini. Tangia App hiyo kuachiwa mpaka hivi sasa imepata kukua kwa kiasi kikubwa sana. Hivi karibuni Google wametangaza kuwa App hiyo watu wameidownload zaidi ya mara milioni 100.
Kulingana na network ya watu waliyo nayo google kwa sasa wanaweza fanya App yeyote kuwa maarufu sana. Hivi unajua Google.Com ndio mtandao unaoongoza kutembelewa na watu duniani? sasa kama ni hivyo itakuaje vigumu wao kutangaza sana huduma zao na kuwafikia watu wengi zaidi. Kuna msemo unasema “Ukishakuwa Baba, Utabaki Baba Tuu”. Hebu tungoje tuone YouTube Music Kama Wataudhihirisha.
One Comment