Ni wazi kwamba soko la simu janja linatawaliwa na chapa nyingi sana za simu za aina mbalimbali na ni wazi kuna zile ambazo zinafanya vizuri kushinda zingine.
Tokea mwaka 2017 mpaka kufikia mwaka huu (500) inaripotiwa kwamba kuna takribani ya chapa (brand) 500 za simu ambazo zinamekufa au kwa namna moja zimetoka katika soko.
Sababu za kutoka katika soko ziko nyingi sana na vipi unakumbauka COVID-19 ilivyofanya yake katika biashara za watu? Sababu ziko nyigi tuu..
Kutokana na ripoti ambayo imetolewa na Counterpoint ambao wamefanya utafiti na kubaini kuwa kuna chapa 500 ambazo zimeachia biashara hiyo tokea mwaka 2017. Kingine cha kushangaza ni kwamba kwa mwaka 2017 kulikua na chapa 700 tofauti tofauti ambazo zilikua zinashindana katika soko la simu janja Kwa mwaka huu chapa ambazo zinachuana katika soko zipo chache sana kwa namba ni 250 tuu, hii ikiwa inaonyesha ni jinsi gani namba hiyo imeshuka.
Lakini pia kuna mambo mengi ambayo pengine yanapelekea namba hii kushuka sio, kuna makampuni ambayo pia yameshindwa kuendana na teknolojia ya sasa mfano 4G kwenda 5G.
Kuna makampuni mengine kama vile Vivo na Xiaomi ambayo yana simu zenye sifa za undani za juu sana lakini zinauzika kwa bei ndogo katika soko, kwa namna moja au nyingine lazima ziwe na ushindani mkubwa katika soko Kwa hali jinsi ilipofikia kama bidhaa ikiwa inafanya vizuri katika soko la simu janja badi ni wazi kabisa kwamba bidhaa hiyo ina vigezo stahiki kabisa.
Kingine nchi kama nchi huwa zinaingilia kati, kama unakumbuka TRCA kuna kipindi walizima simu zote ambazo zilikua hazina viwango (za kichina sana sana) na kuzifanya chapa nyingi kulikosa soko la hapa.
Wengine wanasema bora tuwe wachache lakini twende vizuri kuliko tuwe wengine huku wengine wakiwa ni wasindikizaji huku mara kwa mara wakiharibu njia
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani utafiti huu uko sahihi au unadhani ripoti ina uwalakini kidogo? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn Hash
No Comment! Be the first one.