Kwa mara ya kwanza mtandao wa Snapchat umeshika mioyo ya vijana haswa wale wa miaka 10 mpaka 19. Hapo awali mtandao wa Facebook ndio ulikuwa kila kitu. Kwa sasa utafiti unaonyesha hilo limebadilika
Utafiti huo ulihusisha vijana (10 – 19) 6,500 ambalo walionekana kuwa wanatumia na kuupenda sana mtandao huo. Aslimia 28 kati yao walitoa mawazo yao na kusema wao wanaona huo ndio mtandao wa kijamii ambao ni muhimu sana kuliko yote.
Instagram ilionekana ni muhimu sana kwa baadhi ya vijana ambao waliuchagua mtandao huo katika mitandao mingine yote. Instagram ilipata asilimia 27 kama mtandao muhimu sana, namba hii ikiwa ni nyuma ya Snapchat.
Katika utafiti uliopita vijana wengi (11 – 19) walisema mtandao wa Instagram ndio mtandao mzuri sana na ukashika alimia 33 wakati Snapchat ikishika asilimia 19 tuu.
Ukiangalia namba hizo utaona kuwa Snapchat imeweza kupanda kwa kasi sana. Kitu ambacho pia kionaonyesha mtandao huo unajitahidi katika kukuwa na kwamba wameuboresha mtandao huo sana
Mtandao wa Snapchat tangia uanzishwa kwaka 2011 umeweza kuwapata zaidi ya watu milioni 100 kutembelea App yake. Uwezo wake wa kuwafikia zaidi vijana umeipa umaarufu mkubwa sana. Na kutokana na jambo hilo App hiyo imejikuta ikipata matangazo mengi.
Kutokana na Snapchat, asiliamia 60 ya watumiaji wake wa marekani ni vijana kati ya miaka 13 mpaka 34. Hata video za mtandao huo zinaangaliwa sana kwa siku. Mpaka sasa video zinaangaliwa mara bilioni 8 kwa siku.
Kwa sasa kampuni la Snapchat lina thamani ya dola bilioni 19 za kimarekani, namba hii inalifanya kampuni kuwa moja kati ya kampuni lenye thamani kubwa kati ya mitandao ya kijamii.
Sifa hizo nyingi za Snapchat labda ndio zilizolifanya kampuni hilo kuwa na wapenzi wengi vijana.