Wizi, udukuzi, na utapeli wa mtandaoni ni vitu ambavyo vinaathiri maisha ya mtu na kuweza kuvuruga kabisa amani ya watu au mtu binafsi kutokana na hasara inayosababishwa na udukuzi au utapeli.
Udukuzi au wizi wa kupitia mtandao mara nyingi hufanyika kwa kuiba utambulisho wa mtu (identity) anaotumia kama vile Taarifa za malipo kwa kadi husika (credit card records), Taarifa za utambulisho (Social Security Number) au Taarifa Binafsi mfano namba ya siri, email, namba ya simu n.k

Mfano mtu anapoweza kuiba taarifa za malipo (credit card information) anaweza kuzitumia kwa namna mbili.
Kwanza, anaweza kutumia taarifa hizo kutengeneza taarifa za malipo/bills mbalimbali na kumfanya mtu kuhangaika juu ya bills ambazo anaonekana anadaiwa, mfano unatumiwa bill ya DAWASA ambayo huijui kumbe kuna mtu ametumia taarifa zako kufanya huduma.
Pili, mtu anaweza kutengeneza kadi feki/forgery card ya malipo ambayo inataarifa kama za mtu aliyemuibia taarifa zake na kuanza kuitumia hiyo kadi kufanya malipo ingali hela itakatwa kwenye Account ya yule aliyeibiwa taarifa.
Wizi wa mitandaoni (udukuzi) unaweza kufanyika kwa namna nyingi lakini kwa njia ambazo watu wengi hua wanaathirika nazo ni kama hizi zifuatazo.
1. Kuhadaa (Phishing) : wezi wengi hutuma meseji kwa njia ya SMS au EMAIL ambazo hubeba ujumbe ambao huonekana kama umetoka mahala husika au penye usalama lakini ukikubali kufuata maelekezo ya ujumbe huo basi taarifa zako au vitu vyako huweza kuibwa na wezi (wadukuzi).
Mfano, umepokea Email kutoka kampuni ya Pepsi, Email ya kampuni huwa inafahamika mfano: Sales@Pepsico.com
Ila kama Email ikiwa na vitu vingine, mfano: Sales@Pepsico.js.com basi hapo kuna shida
Au wakati mwingine wanakutumia viunganishi vya tovuti (website links) ambazo siyo za kweli (Fake website links), mdukuzi anatengeneza tovuti/website mfanano na website halali ya kampuni husika ili akushawishi
Mfano: https://www.pespsico.vim. com
Hiyo ni fake website link.
2. Kunakili (Skimming) : Hii hufanyika Zaidi kwenye maeneo kama vile Migahawa/grocery, vituo vya mafuta/oil stations, coffee shops, supermarket n.k ambapo hutumika kifaa maalumu ambacho kinaweza kunakili/copy taarifa zilinazotunzwa kutoka kwenye vitu mbalimbali (Magnetic data). mfano kuna aina ya skimming ambapo hii mtoa huduma kama vile mhudumu/waiter anakua na kifaa cha kunakili/copy taarifa za wateja zilizotunzwa (magnetic data) hivyo ananakili/copy taarifa za malipo za wateja wake ambao wamefanya matumizi kwake na kutumia hizo taarifa kwa dhumuni lake binafsi.
3: Udukuzi wa mtandao (Wi-fi hacking) matumizi ya Wi-Fi ambayo haina ulinzi mzuri hua inawapa urahisi zaidi wadukuzi kutokana na kwamba taarifa za watumiaji zipo wazi kupata na hii zaidi hutokea kwenye sehemu za umma (public Wi-Fi) mfano wa Public Wi-Fi ni kama internet za kwenye migahawa/Restaurant, AirPort, Stendi ya Magari, Hotels n.k
4. Utapeli kwa njia ya simu (Phone scams) : Wadukuzi hutumia njia ya kupiga simu na kuigiza kama wanahusika na mambo kadhaa kama vile ni watumishi wa bank fulani na kuhitaji taarifa fulani kutoka kwako, ukiona simu za aina hii basi tambua ni wadukuzi au kama huamini angalia hiyo namba kisha kata halafu piga tena haiwezi kupokelewa au utaambiwa haipatikani, toa taarifa kwenye Bank husika au mtandao husika.
5: Social Engineering: Hii ni aina ya udukuzi ambapo mtu anakushawishi kwa namna yoyote ile ili aweze kupata taarifa zako binafsi, mtu akipata taarifa zako anaweza kuzitumia kwa mambo yake binafsi kama kufanya miamala au kuiba hela, kuchukua akaunti zako za mitandao ya kijamii, kuuza taarifa zako n.k
Kuwa makini uwapo mtandaoni kwa kuepuka kufungua viambatanisho (attachments), links, au kujibu emails usizokua na uelewa nazo pia unashauriwa kutumia nywila/password ngumu kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii.
No Comment! Be the first one.