Kampuni ya Microsoft watengenezaji wa Windows wametoa bei ya ‘operating system’ yao mpya ya WIndows 8 inayotegemewa kuingia sokoni mwishoni mwa mwaka. Kuna mgawanyo wa bei tofauti tofauti kwa makundi tofauti ya wateja.
Kwa watu wenye kompyuta zenye Windows XP, Vista au Windows 7 na kompyuta zao ni za kisasa watalipa takribani Tsh 62,700/= (kwa kiwango cha dola ya kimarekani kwa sasa) ili kuweza ku’upgrade’ kupitia intaneti kwenda Windows 8.
Na ili kutofanya watu wasinunue kompyuta katika kipindi hiki cha kusubilia Windows 8 Microsoft imetoa punguzo zaidi kwa watu watakaonunua kompyuta mpya ndani ya hichi kipindi hadi hapo Windows 8 itakapotoka. Ukinunua kompyuta mpya ndani ya kipindi hichi utapata punguzo hivyo utatakiwa kulipa dola za kimarekani 14.99 ambazo ni takribani Tsh 23,500/= iliuwezo kui’upgrade’ kwenda Windows 8 kwa kutumia intaneti.
Kwa wale watakaotaka DVD kabisa basi itawabidi kuzama mifukoni zaidi na kutoa $69.99 ambazo ni takribani Tsh 110,000/=.
![]() |
Windows 8 Inategemewa Kuwa Kitu Tofauti Sana Na Windows Zilizopita |
Ila hii ni mara ya kwanza kwa Microsoft kuweka bei ya chini sana, mara ya mwisho ili uweze ku’upgrade’ kwenda Windows 7 ilikuwa itakugharimu $119 kwa Windows 7 Home Edition na $199 kwa Windows 7 Professional.
Je unafikiria kutumia Windows 8? Uta’upgrade’ au unasubiria kompyuta zitakazokuja na Windows 8 kabisa?
No Comment! Be the first one.