WhatsApp Desktop imekuwa mkombozi wa watu wengi ambao kutokana na sababu mbalimbali inakuwa rahisi kwetu kujibu jumbe kwa kupitia kwenye kompyuta hivyo kuifanya simu janja kwenda likizo ya muda 😀 😀 .
Maboresho kadha wa kadha yameshafanyika kwenye WhatsApp Desktop (web) na bado tuu inaendelea kuwekwa vitu vizuri. Sisi ambao tunapenda kufahamu mengi pale tunapotumia programu tumishi (mfano Instagram) tunafahamu kuwa tunaweza kuonyesha hisia kwa kuweka alama ya kupenda (kopa) kutokana na kile ambacho umetuma/kukipokea kutoka kwa mtu mwingine.
Basi kitu hicho kipo mbioni kwenda kwenye WhatsApp Web ambapo kwa sasa kipo kwenye hatua ya matengenezo ambapo mtu ataweza kuweka alama ya kopa kama ishara ya kuonyesha kuwa amependezwa na kile ambacho amekipokea/amekituma. Hii ni sawa tuu kama ambavyo inawezekana kufanya hivyo kwenye Instagram.

Kuhusu ujio wa maboresho haya bado haijulikani na kwa sasa kipengele hicho kipya kipo katika hatua ya kutengenezwa na haijulikani ni lini kitaletwa kwa watumiaji kwa majaribio au kuanza kupatikana kwa watu wote wanaotumia WhatsApp Desktop.
Kwa hakika kuonyesha kuwa sisi ambao tunapenda kutumia WhatsApp kwa njia ya kompyuta tunazidi kufurahi tuu kwani inatusaidia kufanya vitu vingi bila ya kupata adha ya kushika simu janja unafikiri kitu gani kikiletwa kwenye WhatsApp web kitakufurahisha sana?
Chanzo: WaBetaInfo
One Comment