Jopo la madaktari watafiti linataka kuwarudishia uhai tena watu wanafariki kutokana na magonjwa yanahusisha ubongo. Baada ya utafiti wa muda mrefu sasa wapewa leseni ya kuruhusu kuweza fanya majiribio.
Fikiria uwezekano wa kurudisha uhai kwa watu waliofariki kutokana na matatizo ya ubongo… hicho ndicho shirika la Bioquark linataka kufanya
Bodi ya masuala ya afya ya Marekani imekubali ombi la shirika la Bioquark la nchini humo ambalo ndilo limejikita katika kufanya majaribio ya kurudisha hai ubongo wa mtu ambao ulikuwa ume’kufa’ kutokana na hitilafu za magonjwa kama vile saratani (kansa).
Shirika hilo la “Bioquark” limepewa ruhusa ya kuendelea na utafiti huo uliopewa jina la “ReAnima Project” na kwa kufanikisha hilo kampuni hiyo iko mbioni kufanyia utafiti maiti 20 waliokufa kutokana na kansa ya ubongo ili kuweza kufanikisha project hiyo.
Utafiti huo utajumuisha kwa majaribio ya kushtua ubongo kwa kupandikizwa “Stem cells” kwenye ubongo pamoja na dawa zinazouwa wadudu “Pesticides”. Pamoja na hayo, utafiti huo utajumuisha kushtua neva na kutumia “lasers” kuweza kushtua ubongo.
Jopo hilo la madaktari lina matumaini kuwa seli zilizopandikizwa kwenye ubongo zitaanza kufanya kazi kama mwendo wa “Robot” na baada ya muda mfupi ubongo wenyewe utakuwa na uwezo wa kuzalisha seli hizo na hivyo kuweza kufanya kazi bila msaada, hii ni sawa na wale wanyama walio kwenye kundi la reptilia kuweza kuota kiungo baada ya kupata dhoruba ya kukatwa na kupata tatizo la aina nyingine.
Matokeo ya awali ya utafiti huo yanatarajiwa kutoka miezi miwili baada ya utafiti huo kuanza na ni matumaini ya wengi kufanikiwa kwa utafiti huo kutaweza kurudisha furaha kwa wale watakaoweza kupata huduma hiyo na kuweza kuwaona ndugu/rafiki wakiwa hai na kuweza kufanya shughuli zao za kila siku.
Soma pia – Oparesheni ya Kuunganisha Kichwa na Kiwiliwili mbioni kufanyika…
Je watafanikiwa? Endelea kutembelea TeknoKona, tutaendelea kufuatilia na kukupa habari pale zikipatikana.
Chanzo: Fortune.com na mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.