Pengine hili sio jambo geni sana katika mtandao wa WhatsApp sababu mpaka sasa kuna huduma ya ku’share status kutoka katika mtandao wa WhatsApp na kwenda Facebook moja kwa moja.
Kufanikisha hili ni jambo dogo ili kuweza kupeleka status hizo za WhatsApp moj akwa moja katika mtandao wa Instagram.
Kingine ni kwamba tokea mwanzo hili lilikua linajulikana tuu kwamba liko njiani maana mtandao wa Meta uliweka wazi kwamba unatafuta njia ya kuinguanisha mitandao yake ya kijamii.
Sio lazima uingia katika kila mtandao ili kuweka status, unaweza kutumia mtandao wa WhatsApp na kuamuru status hiyo hiyo iende katika mitandao mingine (Facebook na Instagram).
Kumbuka kipengele hiki sio cha lazima na ni wewe mwenyewe tuu utaamua kama unataka kupeleka moja kwa moja status hiyo katika mitandao hiyo ya kijamii au laa.
Kipengele hiki kimeonekana katika toleo la majaribio la WhatsApp Beta ya Android 2.23.25.20 na ni wazi kwamba kitaanza kupatikana katika siku zijazo.
Lakini kingine ni kwamba kuna baadhi ya vipengele ambavyo viko katika mtandao wa Instagram na havipatikani katika mtandao wa WhatsApp.
Vipengele hivyo vingi ni katika eneo la uhariri (Edit). Mfano kama una video/picha yako ambayo ulikua unataka uihariri (edit) kabla ya kuisambaza katika mtandao wa Instagram…
….itashindikana kama ukitumia mtandao wa WhatsApp moja kwa moja, maana kule itaenda kusambazwa tuu
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je utakua ni mtumiaji mzuri wa kipengele hiki?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.