Spotify ni programu tumishi ambayo ina nyimbo za wasanii mbalimbali kutoka dunia nzima lakini pia inafanya kazi kwenye saa janja za Apple (Apple Watch).
Spotify ambayo inawatumiaji wengi tuu duniani na hata hivi karibuni programu tumishi husika imeweza kupatikana nchini Tanzania kama ambavyo tuliwahabarisha. Muziki ni kiburudisho cha wengi duniani kwa taarifa tuu Spotify imeboreshwa.
Watu wengi wanatumia muziki kama burudani wakati wanapofanya mazoezi lakini hebu fuatilia mfano huu: umetoka mahali unapoishi kwa ajili ya kwenda kupasha viungo vyako vya mwili na baada ya kukimbia umbali mrefu kidogo unajikuta kuwa ulisahau kubeba simu janja ama kifaa kingine kwa ajili ya kupata burudani, naamini utakuwa mpweke lakini Spotify imeboreshwa!
Katika maboresho ambayo yamefanyika kwenye Spotify sasa mtu anaweza kushusha nyimbo mbalimbali kupitia saa janja (Apple Watch). Hii maana yake ni nini? Jibu ni si lazima tena kutegemea simu janja kuweza kuburudika kwa muziki wakati umeenda kufanya shughulu mbalimbali mathalani michezo.
Spotify yaboreshwa: Sasa inawezekana kushusha nyimbo na kusikiliza kupitia saa janja za Apple.
Habari ya uwezo wa kushusha nyimbo kwenye Spotify inaweza kuwa ni ya furaha kwa wengi lakini maboresho hayo ndio kwanza yametoka hivyo haijapatikana kwa wote. Sisi neno letu ni moja tu nalo ni usisite kutufuatilia kila siku kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.