Moja ya njia rahisi siku hizi kutumia WhatsApp kiraisi hasa kwa sisi ambao kazi zetu zinategemea matumizi ya kompyuta ndio shughuli ikamilike ni WhatsApp Desktop (web) ambayo kimsingi imekuwa ikiboreshwa na kufanya ifanane karibu kabisa kama ile ya kwenye iOS/Android.
Mimi ni mmoja ambae natumia WhatsApp ya kwenye mtandao kupitia kwenye kivinjari kila siku na imekuwa msaada sana kwangu kutokana na kutokuwa na ulazima ili jumbe ziweze kuingia na kutoka na haya ni maboresho ambayo watu wengi wanatumia njia hii ya mawasiliano wanaifurahia lakini si kwamba anayetumia njia hii ya mawasiliano basi simu janja inakuwa si ya lazima tena, la hasha!
Hilo ni moja tu kati ya mengi ambayo yameboreshwa kwenye WhatsApp Desktop, kingine ni uwezo wa mtumia kuweza kushusha ripoti ya matumizi yake ya WhatsApp Web; mtumiaji wa WhatsApp anaweza kuomba ripoti ya vitu ambavyo amevifanya katika kipindi fulani.
Ripoti hii inaweza kushushwa baada ya mtu kupeleka maombi WhatsApp na mchakato kuanza kisha baada ya saa 24 mtu kuweza kuishusha. Uwezekano wa mtumiaji kuweza kushusha ripoti ya yale ambayo ameyafanya kwenye WhatsApp katika kipindi fulani ilikuwa inawezekana kwenye Android/iOS tu lakini sasa kipengele hicho kimefika kwenye WhatsApp ya mtandaoni.
Uwezo wa kushusha ripoti ya vitu ambavyo mtu amevifanya kwenye WhatSApp katika kipindi fulani ulianza mwaka 2018 kwa upande wa Android na iOS. Kwa wale ambao wameshawahi kupeleka maombi ya kutaka kutengenezewa ripoti wanafahamu uzuri wake.
Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali
One Comment