Kutokana na utandawazi, ukuaji wa teknolojia watu tunaweza kuvutiwa na kifaa (simu janja, tabiti, n.k) hivyo kusababisha kununua bidhaa hiyo na tunapokuja kufanya usajili kwenye WhatsApp kwa mara nyingine tena kutokuta mazungumzo ni jambo la kawaida sana.
Inawezekana tusiwe wengi ambao tunapenda kutopoteza mazungumzo ya WhatsApp na hii inatokana na sababu mbalimbali. Vilevile, unaweza ukawa ni mhanga ambae ulishawahi kujikuta mawasiliano na ndugu, jamaa yametoweka mara baada ya kusajili namba yako ileile ya WhatsApp lakini sasa kwenye simu tofauti.
Suala hilo sasa linafikia ukomo kulingana na WABetaInfo ambapo mtumiaji wa WhatsApp atakuwa na uwezo wa kutopoteza mazungumzo yake hadi kufikia vifaa vinne yaani mtu akiamuru kitu kifanyike kwenye kifaa kimoja kwa wakati huohuo (synchronise chat) taarifa zile zitakuwa zimejirekodi kwenye WhatsApp ya akaunti sawa kutoka kwenye rununu, tabiti. Kwa lugha rahisi ni kwamba mtu ataweza kutumia mpaka akaunti nne (4) kwa namba ileile bila kutopteza mazungumzo.

Pia, maboresho hayo kuna uwezekano wa WhatsApp Web kuweza kujitegemea yenyewe bila WhatsApp ya kwenye simu janja kuwa hewani.
Yapo mengi ambnayo yanatazamiwa kuja kuhusu programu tumishi yenye watumiaji wengi zaidi, kazi yetu ni kusubiri na kama kawaida yetu tutaendelea kuwahabarisha kama kawaida yetu.
Daima tunafurahia maoni yenu hivyo basi usisite kutuandikia kupitia kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii.
Vyanzo: WABetaInfo, Gadgets 360