WhatsApp ni mtandao wa kijamii ambao mara kwa mara unakuja na vipengele kadha wa kadha ili kuhakikisha kwamba wanabaki kuwa juu katika kurahisisha mawasiliano.
WhatsApp ni moja kati ya njia rahisi kabisa katika kufanya mazungumzo ya papo hapo na ni moja kati ya mitandao ya kijamii maarufu sana.
Lakini nadhani umeshawahi kuwaza kutumia akaunti mbili (namba mbili tofauti za simu) katika WhatsApp moja kama ilivyo katika mitandao mingine ya kijamii?
Hili WhatsApp wanakuja na suluhu yake maana wametangaza kwamba watakuja na sasisho (update) ambalo litakua na kipengele hicho ambacho kitawezesha kutumia namba mbili za simu ndani ya WhatsApp moja.
Kinachofanyika ni kwamba kutakua na namna ambayo utaweza kuchagua ni akaunti (namba) gani ambayo utaweza kutumia kwa muda huo kwa mfano kujibia meseji zako.
Ni wazi kabisa kwamba hii inapendeza maana kuna watu wenye akaunti mbili na moja inakua ni ile binafsi huku nyingine ikiwa ni ya biashara.
Lakini hapa ni lazima kwanza uwe na namba mbili au uwe na simu ambayo inakubali laini mbili ili kuweza kupokea zile namba za PIN (code) za mwanzo kabisa ukiwa unajiunga
Ukikamilisha hilo utakua na uwezo wa kutumia namba zako zote mbili katika WhatsApp moja bila ya wasiwasi wowote.
Hili lilikua linasubiriwa kwa muda tuu maana wengi wamekua wakitaka kupata uwezo wa kutumia namba nyingi katika WhatsApp moja.
Hili ni jambo zuri sana kutoka kwao Meta
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.