Maji ya kunywa ambayo ni muhimu sana kuzidi hata chakula. Imegundulika njia mpya na rahisi ya kupata maji ya kunywa hewani (in the air). Haina haja ya kushangaa kwani hiyo ndio sayansi na teknolojia inayokuja na mapya kila siku.
Wanasayansi wametengeneza kifaa kichotumia umeme wa Jua ambacho kina uwezo wa kubadilisha unyevu kutoka angani na kuwa maji. Kwa majaribio yaliofanyika katika chhuo cha MIT kifaa hicho kidhihirisha kuzalisha karibu birauli moja kwa kiasi cha 20%-30% cha unyevu (humidity) kutoka angani.
Kinafanyaje kazi?
Ni wazi kuwa teknolojia ya umeme wa Jua inapendwa na inashauriwa na wengi kutumiwa na wengi kutokana na kuwa si ghali na pia haichafui mazingira. Kifaa hicho wakati wa usiku kwa mchanhanyiko wa Zirconium na asidi ya Adipic na kinavuta vimelea vya maji vilivyopo hewani kisha mchana kwa mguvu Jua na kuvipooza na kufanya kuwa maji salama kabisa kwa kunywa.
Wanasayansi bado wapo katika hatua ya majaribio na kifaa hiki hakipatikani popote kule kutokana na kwamba bado kipo katika hatua ya majaribio.
Changamoto?
Kila kitu kina chasngamoto zake na katika hali ya kufanikisha kifaa hicho kinazalisha maji salama ya kunywa ni gharama za juu za Zirconium hataa hivyo wanasayansi wanasema wamepata uvumbuzi wa suala hilo na kutumia Aluminum ya bei rahisi.
Wanasayansi teknolojia hii inaweza kuja kuutmia na wengi kutokana na urahisi wake ukizingatia 1 kati ya watu 10 wanakosa maji ya kunywa na 88% ya magonjwa yote yanatokana na watu kutokunywa maji yaliyo safi na salama.
Teknolojia hii inaweza kuwa mkombozi kwa zile nchi ambazo kwa muda mrefu zinakuwa na ukame ambapo kifaa hicho kitawawezesha kupata maji ya kunywa yaliyo salama kwa kunywa.
Vyanzo: Fortune, The Sydney Morning Herald
One Comment
Comments are closed.