Ni Disemba na hiki ndio kipindi ambacho kumi bora za mwaka huwa hazikauki kila kitengo, leo nitakuletea video maarufu zaidi katika tovuti maarufu ya YouTube kwa mwaka 2015.
Video hizi kumi maarufu zaidi zimeamuliwa na YouTube wenyewe kutokana na marangapi video imeangaliwa, ilipokelewaje? na ilisambaaje.
YouTube huwa wanataja video hizo marufu katika chaneli yao inayokwenda kwa jina la YouTube Rewind.Video hizi za maarufu za mwaka 2015 zimegawanywa katika makundi mawili, moja ni ya video za muziki na kundi la pili ni video za kawaida kama matangazo ucheshi na vipindi vya television.
Video maarufu zaidi za upande wa muziki.
Wimbo huu uliotumika katika filamu maarufu ya Fast Furious 7 ya mwaka 2015, na ulipendwa zaidi kwa kuwa uliimbwa kama kumbukumbu ya Paul walker mmoja wa wacheza filamu hiyo aliyefariki dunia mwaka 2013 wakati filamu hii ikitengenezwa.
Video ya wimbo huu imeangaliwa zaidi ya mara bilion moja.
Hii ni video maarufu namba mbili kwa mwaka huu wa 2015 na mpaka sasa imekwisha tazamwa karibu mara milion miatisa ishirini. Sugar ni wimbo ulio katika album ya tano ya studio ya bendi hiyo kutoka nchini Marekani, hii albamu ilirekodiwa mwaka 2014 na video ili chapishwa mwezi Januari.
3. Ellie Goulding – Love me like you do.
Huu ni wimbo unaotoka katika ablamu ya DELIRIUM ya msanii Ellie, video hii ilichapishwa mwezi January mwishoni na mpaka sasa imekwisha tazamwa zaidi ya mara milioni mia nane na hamsini.
4. Major Lazer & DJ snake – Lean On
Hii ni video ilichapishwa YouTube mwezi wa tatu mwishoni na ikaweza kujipatia umaarufu kwa kasi, mpaka sasa imekwisha tazamwa zaidi ya mara milioni mia tisa.
Katika nafasi ya tano anasimama Taylor Swift na video ya wimbo wake Bad blood ambao umetazamwa zaidi ya mara milioni mia sita tangu ilipochapishwa hapo mwezi Mei.
Hey Mama ni video maarufu namba sita ambayo tangu ilipochapishwa imeweza kutazamwa zaidi ya mara milioni miatano, video ya wimbo huuu imechapichwa YouTube mwezi Mei
Ingawa video hii ilipigiwa kelele na watetea haki za watoto baada ya kumuonesha mtoto akipigana ndani ya banda lakini hilo halikuizuia kuweza kuangaliwa zaidi ya mara milioni mia nne sabini tokea ilipochapishwa mwezi wa Januari.
Hii ni video kutoka kwa kundi ambalo lilitokana na kipindi cha runinga cha kutafuta vipaji cha X factor, wakimshirikisha msanii kid ink wameweza kutazamwa zaidi ya mara milioni mia nne tisini. Ingawa video yao imetazamwa zaidi na mtandaoni kushinda video iliyopo namba saba hii ni kwa sababu kigezo sio tuu marangapi video imetazamwa mtandaoni.
Ikiwa haina wiki nyingi tangu iwekwe mtandaoni mwezi Oktoba video hii ya mwanadada Adele imekwisha tazamwa zaidi ya mara milionI mia Saba. Huu ni wimbo kutoka katika albamu mpya ya adele inaitwa 25.
10. Silento – Watch me
Wengi wanaujua huu wimbo kama whip Nae Nae, ni wimbo uliojipatia umaarufu hasa kwa staili za uchezaji zinazoonyeshwa na wahusika. tangu kuchapishwa imekwisha tazamwa zaidi ya mara milioni mia nne themanini.
Je ni video gani ya mwaka huu iliyopo YouTube ungefurahi kama ingeingia kwenye orodha hii?
No Comment! Be the first one.